REAL MADRID WAPATA MSIBA MZITO,
ULIMWENGU
wa soka umepata pogo kufuatia kifo cha gwiji wa Real Madrid,
mshambuliaji Alfredo Di Stefano aliyefariki dunia akiwa ana umri wa
miaka 88.
Mwanasoka
huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Argentina na Colombia
aliopatwa na ugonjwa wa moyo karibu na Uwanja wa klabu hiyo, Bernabeu
Jumamosi mchana na akafariki dunia mchana wa leo.
Bingwa wa Ulaya: Alfredo di Stefano wa Real Madrid akiwa na makombe matano ya Ulaya, amefariki dunia leo
Pigo
kubwa: Gwiji wa Real Madrid, Alfredo Di Stefano akisherehekea na Kombe
halisi la Ulaya baada ya Real kuifunga Reims 4-3 katika fainali mwaka
1956 mjini Paris
WASIFU WA DI STEFANO
1945–1951 River Plate Mechi 66 Mabao 49
1951–1953 Millonarios Mechi 102 Mabao 90
1953–1964 Real Madrid Mechi 282 Mabao 216
1964–1966 Espanyol
Mechi 47 Mabao 11
Rais
huyo wa heshima wa Real Madrid aliwekwa chumba cha wagonjwa maalum,
akipatiwa tiba makini, lakini haikusaidia kuirejesha hali yake vizuri.
Amekuwa katika hali mbaya mno tangu Jumamosi alipofikishwa hospitali ya General Universitario Gregorio Maranon mjini Madrid.
Jitihada
za madaktari bingwa wa hospitali hiyo kuokoa maisha ya gwiji hiyo
hazikufanikiwa na hatimaye mchana wa leo akaaga dunia. Kikosi cha
magwiji wa Real Madrid kinatarajiwa kuwa na ziara nchini mwezi ujao kwa
mwaliko wa makampuni ya TSN, chini ya Mkurugenzi wake, Farough Baghozah.
Pumzika
kwa amani gwiji: Di Stefano hapa akiinua bilauri yake wakati wa hafla
maalum ya kumuenzi kwa mchango wake katika soka, iliyofanyika Ubalozi wa
Argentina mjini Madrid. Ndiye mfungaji bora wa pili kihistoria Real
Madrid.
0 comments:
Post a Comment