Thursday, 17 July 2014

LOUIS VAN GAAL: SIKU YA KWANZA MAZOEZINI CARRINGTON!


>>ZOEZI MARA 2 KWA SIKU, CHAKULA PAMOJA VIKOSI VYOTE!
>>LEO VAN GAAL KUTAMBULISHWA RASMI, KUONGEA NA WANAHABARI!
Louis van Gaal alitua Jana Asubuhi Jijini Manchester na moja kwa moja kwenda huko Aon Training Complex, Carrington kupokea taarifa toka kwa Wasaidizi wake Ryan Giggs, Albert Stuivenberg na Marcel Bout ambao walikuwa Mazoezini na Timu tangu Julai 4.
Van Gaal alisimamia Mazoezi mwenyewe Jioni kuanzia Saa 1 na Nusu Usiku, Saa za Bongo.
MANUNITED-GIGGS-LVG-WOODWARDMara baada ya kupokea Taarifa kwa Wasaidizi wake, Van Gaal aliongea na Mchezaji mmoja mmoja baada ya Mazoezi ya Asubuhi lakini ameamua kuongea na Kikosi chote kwa pamoja baada ya Timu kukamilika watakapojiunga Wachezaji ambao bado wapo likizo kwa vile walikuwa Brazil na Timu zao za Taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Moja ya mabadiliko makubwa aliyoleta Van Gaal, tofauti na Sir Alex Ferguson na David Moyes, ni uamuzi wake kwamba Makocha wote, Wachezaji wote wa Kikosi cha Kwanza na cha Pili lazima wajumuike pamoja wakati wa Chakula cha Mchana.
Kitu kingine ni uamuzi wake kwamba Mazoezi yawe mara mbili kwa Siku na baada ya yale ya Asubuhi pamoja na Chakula cha Mchana, Wachezaji walikuwa na uamuzi wa kubaki Carrington au kwenda Makwao kupumzika ili kurejea Jioni kwa Raundi ya Pili ya Mazoezi.
Inaaminika moja ya mambo yaliyogusiwa kwenye Mkutano na Wasaidizi wake ni ile haja ya haraka ya kupata wapya kwenye nafasi za Sentahafu na Kiungo wa Kati.
Pia, inasemekana Wachezaji wenye Mikataba ya chini ya Miaka miwili nao atawatupia jicho kali kuona wanastahili kubaki au kuuzwa.
Miongoni mwa hao ni pamoja na Chris Smalling, Tom Cleverley, Javier Hernández, Shinji Kagawa, Darren Fletcher na Ashley Young.
Wengine ambao watakuwa kwenye darubini kali ni wale waliokuwa nje kwa Mkopo ambao ni pamoja na Anderson, Bebe, Nick Powell, Jesse Lingard, Wilfried Zaha na Rodriguez.
Leo Jioni, Van Gaal atatambulishwa rasmi na kisha kuongea na Wanahabari kwa mara ya kwanza.
Ijumaa ataruka na Kikosi cha Man United kwenda kupiga Kambi huko California na kucheza Mechi yao ya kwanza hapo Julai 23 dhidi ya Los Angeles Galaxy.
USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:
[Zote Nchini Marekani]
**Saa za Bongo
Jumatano 24 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
0606 Manchester United v LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
2306 Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumanne 30 Julai 2014 [Usiku wa 29 kuamkia 30], FedEx Field, Washington DC
0230 Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumanne 02 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor
2306 Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumanne 12 Agosti 2014, Old Trafford
REUNITED14
2130 Manchester United v Valencia

Related Posts:

0 comments: