James Mwakibinga (27) mkazi wa kijiji cha iwambala kata ya
Igawilo Wilayani Mbeya Ameshitakiwa kwa
balozi wa mtaa huo baada ya kumpiga mke
wake Anaye julikana kwa Jina la Salome Mwaipopo.
Akiongea Na Mtandao Huu Bi Salome
Mwaipopo amesema kuwa ameamua
kumshitaki James kwakuwa ana mpiga mara
kwa mara na anamsababishia majeraha ya mwili hali ambayo niunyanyasaji wa
kijinsia,pamoja na hayo Bi Salome
Mwaipopo ameongeza kuwa amemshitaki kwa Balozi ili apate Barua ya kumpeleka
Polisi mumewe kwakuwa amezoea
kumnyanyasa bila sababu ya msingi.
Aki thibitisha kwa tukio hilo Balozi wa mtaa
huo Mapinduzi Mwaipopo amesema Amepokea
malala miko hayo kutoka kwa mke wa James anaye daiwa kufanyiwa ukatiri wa
kijinsia ,Balozi ameongeza kuwa hua akipokea malala miko kutoka kwa mwanamke
huyo mara kwa mara na kumuonya James kutokana na tabia yake hiyo ya kumpiga
Mkewe .
Hivyo
balozi wa mtaa huo ametoa wito kwa
wanaume wasiwe na tabia za kuwa nyanyasa
wake zao kwa sababu nao wana haki ya kuishi na kufanya maamuzi .
Kwaupande wake Samsoni Mwakibinga Ambaye ni mdogo wake na
James amesema kuwa wame choshwa na tabia ya kaka yao yakumpiga na kumnyanyasa mke
wake bila sababu za msingi ni bora
apelekwe polisi wa iliakajifunze
tabia.
Mwandishi.
Abdul Marwa Mbeya greenews.blogsport.com
0 comments:
Post a Comment