Mkurugenzi
wa Mikono Business Consult Themi Rwegasira akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina maalum ya
uongozi bora itakayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 13
Juni, pembeni yake wa kwanza kulia ni msemaji wa siku hiyo Brian
Tracy,Mkurugenzi mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius
Kilawe(katikati) na Azim Jamal msemaji kutoka Canada.
………………………………………………………………….
Wasemaji
mashuru katika masuala ya uongozi bora na maendeleo Bw.Brian Tracy
kutoka Marekani na Azim Jamal kutoka Canada wataongoza semina maalum ya
uongozi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Juni 13 kwa vijana wa
Kitanzania.
Wakiongea
na waandishi wa habari leo jijini dare s Salaam wataalum hao wemesema
ni muhimu kuwepo kwa semina hiyo ambayo itawasaidia vijana katikati
uongozi na hivyo kuwa na fursa nzuri ya kuajiriwa katika ngazi za juu
badala ya kuwapa wageni nafasi hizo,
“Ni
vizuri kuhudhuria semina hii kwasababu kupitia semina hii ina mafunzo
mazuri kuhusu uongozi bora kwa kupata mbinu muhimu za uongozi bora
kuanzia ngazi ya kampuni hadi ya Taifa hivyo” alisema Brian
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mikono Business Consult aliongeza kwa kusema semina
hii itasaidia kuleta maendeleo katika nchi yetu hususani katika nyanja
ya uongozi kwa kuweza v kuwa na viongozi bora wa baadaye watakaofuata
taratibu,kanuni na sheria za uongozi katika sehemu zao za kazi.
“kama
ukiangalia katika Makampuni makubwa na Taasisi za kifedha utaona kuwa
ni watanzania wazawa wachache tu ndio wako katika ngazi za juu za
uongozi ambapo asilimia 96 ni wageni na asilimia 4 ndio wazawa kupitia
semina hii itabadilisha utaratibu kwa kuwa na asilimia kubwa ya wazawa
katika uongozi wa juu.” Alisema Deogratius
Semina
hii inawalenga watu wote kutoka katika sekta binafsi, sekta za
umma,taasisi za kijamii,makampuni ya umma,viongozi wa Kiserikali pamoja
na wale wote waliokatika uongozi ili kuweza kujijenga zaidi katika
enao la uongozi na kupata matokeo mazuri yenye kuleta maendeleo kwa
jamii yetu ya Tanzania.
Vilevili
Bw. Brian Tracy ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kimataifa
ya Brian Tracy ambayo inajishughulisha na kutoa mafunzo ya maendelao kwa
watu mbalimbali,vilevile ameweza kusaidia makampuni 1000,na kuongea na
watu milioni tano katika nchi arobaini duniani,pia ameweza kuandika
vitabu 45 katika lugha mbalimbali.
Naye
Azim Jamal ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc
kampuni inayojishughulisha na kusaidia wadau na makampuni kupata
stahiki katika kazi zao,na ni mwandishi wa vitabu mbalimbali
vilivyotafsiriwa katika lugha 10.
Habari na Lorietha Laurence-Maelezo
0 comments:
Post a Comment