Thursday, 12 June 2014

KOMBE LA DUNIA: TATHMINI MECHI 3 ZA IJUMAA! MEXICO v CAMEROON, SPAIN v HOLLAND, CHILE v AUSTRALIA!

JUMAA, JUNI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Mexico v Cameroon
A
Estadio das Dunas
2200
Spain  v Netherlands
B
Arena Fonte Nova
0100
Chile  v Australia
B
Arena Pantanal
Spain v Netherlands
ROBBEN_v_PIQUEIjumaa, Spain wanaanza utetezi wa Taji lao la Ubingwa wa Dunia kwa kucheza na Netherlands ambao ndio walikuwa Wapinzani wao kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Miaka Minne iliyopita iliyochezwa huko Johannesburg, Afrika Kusini na Spain kushinda Bao 1-0.
Safari hii, Spain wanatinga wakiwa na Kikosi chao karibu chote cha Miaka Minne iliyopita lakini Netherlands wamebakiwa na Wachezaji 7 tu wa wakati huo.
Spain ina Kikosi ‘kilichozeeka’ na, bila shaka, kwa kina Xavi, Iker Casillas na David Villa, hii ni Fainali yao ya mwisho.
Lakini pia wanao Chipukizi kama vile Koke, alieisaidia sana Atletico Madrid kutwaa Ubingwa wa La Liga, ambae haya ndio Mashindano yake ya kwanza makubwa.
Spain pia wanae Straika hatari wa Atletico Madrid Mzaliwa wa Brazil, Diego Costa, ambae ameikana Nchi yake ili achezee Spain na yeye pia haya ni Mashindano yake ya kwanza makubwa.
Lakini Netherlands, chini ya Kocha Louis van Gaal anaehamia Manchester United baada ya Fainali hizi, wana Fowadi hatari mno inayoogopewa huko Ulaya.
Wanao Arjen Robben, Robin van Persie na Wesley Sneijder ambao ni wazoefu na denja kwenye kuona nyavu.
Uso kwa Uso
-Mechi: 9
-Spain: Ushindi 4
-Netherlands: Ushindi 4
Sare: 1
VIKOSI VINATARAJIWA:
Spain: Casillas, Ramos, Pique, Alba, Martinez, Fabregas, Alonso, Iniesta, Silva,  Costa, Villa
Netherlands: Cillessen; Blind, Indi, de Vrij, Vlaar, Janamat; de Jong, Sneijder, Guzman; Robben, Van Persie
REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
Chile v Australia
Chile, chini ya Kocha Jorge Sampaoli, wanapewa nafasi na baadhi ya Wachambuzi lakini wapo Chile_v_Australiakwenye Kundi gumu pamoja na Spain na Netherlands na Mechi hii na Australia ni lazima washinde ikiwa watataka kusonga.
Mashambulizi ya Chile ni ya kushtukiza na huongozwa na Wachezaji wa Klabu za Spain, Eduardo Vargas wa Valencia na Alexis Sanchez wa Barcelona.
Tangu mwanzoni mwa 2013, Chile wamepoteza Mechi 3 tu katika Mechi 18.
Australia wana Rekodi mbovu kwa Mwaka 2014 kwani hawajashinda hata Mechi moja kati ya 3 walizocheza na Kocha Ange Postecoglu anatinga huko Brazil akiwa hajawahi kucheza Mechi ya Mashindano rasmi na Timu hiyo ambayo Wachezaji tegemezi kwao ni Mile Jedinak wa Crystal Palace na Mchezaji wa zamani wa Everton Tim Cahill.
Uso kwa Uso
Chile 2 Australia 1, Kirafiki Februari 2000
Australia 0 Chile 1, Kirafiki Februari 1998
Chile 3 Australia 0, Kirafiki Aprili 1996
-Chile 0 Australia 0, Kombe la Dunia 1974
Dondoo Muhimu:
-Chile hawajafungwa na Australia katika Mechi 4.
-Mara pekee Chile na Australi zimekutana kwenye Kombe la Dunia ni Mwaka 1974 na kutoka 0-0.
-Mchezaji pekee wa Australia anaechezea Ligi Kuu England ni Mile Jedinak na Chile hawana hata mmoja.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Chile: Bravo (Nahodha); Isla, Medel, Jara, Mena; Gutierrez, Aranguiz, Diaz, Valdivia; Sanchez, Vargas.
Australia: Ryan; Franjic, Spiranovic, Wilkinson, Davidson; Jedinak (Nahodha), Miligan, Bresciano; Leckie, Oar, Cahill.
REFA: Noumandiez Doue [Ivory Coast]
Mexico v Cameroon
CAMEROON-ETOHii ni Mechi muhimu mno kwa Timu hizi mbili hasa kwa vile Wapinzani wao katika Mechi inayofuatia ni Brazil na Croatia.
Kocha wa Mexico, Miguel Herrera, anatarajiwa kumuanzisha Kipa Guillermo Ochoa na Mastraika Oribe Peralta na Giovani dos Santos huku Staa wa Manchester United, Javier Hernandez ‘Chicharito’ akianzia Benchi.
Wachezaji wa Cameroon, baada ya kugoma huko Nchini kwao wakiwa na mvutano wa Malipo ya Bonasi na Uongozi wao, hatimae walikubali kusafiri kwenda Brazil wakichelewa kwa Masaa 12.
Chini ya Kocha Mjerumani Volker Finke, Cameroun watategemea sana uzoefu wa Straika Samuel Eto’o, ambae hana Klabu baada kumaliza Mkataba na Chelsea, pamoja na Eric-Maxim Choupo-Moting, Straika anaechipukia kutoka Mainz, na Kiungo wa Barcelona Alex Song, alietokea Arsenal.
Uso kwa Uso
Mexico 1 (Guzman) Cameroon 0, Kirafiki Septemba 1993
Dondoo Muhimu:
-Mafanikio makubwa kwa Mexico kwenye Fainali za Kombe la Dunia ni Miaka ya 1970 na 1986, zote zikichezwa Nchini kwao, walipofika Robo Fainali.
-Cameroon ndio Nchi ya kwanza toka Afrika kuweza kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia huko Italy Mwaka 1990 wakati Straika wao Roger Milla alipoweka Rekodi ya kuwa Mchezaji ‘Mzee’ aliefunga Goli kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Mexico: Corona, Aguilar, Rodríguez,  Márquez, Moreno, Layún, Vázquez, Guardado, Herrera, Peralta, dos Santos
Cameroon: Itandje, Djeugoue, Bedimo, N’Koulou, Song, Mbia, Enoh, Matip, Choupo-Moting, Moukandjo, Eto’o
REFA: Wilmar Roldan [Colombia]
KOMBE la DUNIA
RATIBA-Mechi za Ufunguzi:
[Saa za Bongo]
Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A
2300 Brazil v Croatia
Ijumaa 13 Juni 2014
1900 Mexico v Cameroon
KUNDI B
2200 Spain v Netherlands
0100 Chile v Australia

Related Posts:

0 comments: