Sunday, 1 June 2014
HOME »
» GHANA YATAJA KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WATAKAO CHEZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL,
GHANA YATAJA KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WATAKAO CHEZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL,
Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 11: 45 jioni
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zinazoanza kushika kasi mwezi huu nchini Brazil.
Kikosi hicho cha Appiah kinajumuisha wachezaji 16 wanaokwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza, huku nahodha Asamoah Gyan na Sulley Muntari wakiwa wakongwe wanaokwenda kucheza fainali zao za tatu mfululizo, wakati Jonathan Mensah, Michael Essien, Kwadwo Asamoah, Andre Ayew na Kevin-Prince Boateng wanakwenda kucheza fainali hizo kwa mara ya pili.
Kocha huyo mwenye miaka 53 amewaacha majeruhi Jerry Akaminko, Jeffrey Schlupp na David Accam katika kikosi hicho kinachoelekea Miami kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ambapo kitacheza mechi ya kirafiki juni 9 dhidi ya Korea kusini
Akaminko alipata majeruhi jana jumamosi katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kirafiki na atafanyiwa upasuaji utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa miezi mitatu.
Ghana iliyofika robo fainali mwaka 2010 ipo kundi G pamoja na nchi za Marekani, Ujeruman na Ureno.
Kikosi kamili:
Walinda Mlango:Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars)
Mabeki: Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege/Porto), Harrison Afful (Esperance), John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns)
Viungo: Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan)
Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux
0 comments:
Post a Comment