Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Sadiq al Mahdi amekamatwa kutokana na madai ya kuchochea chuki dhidi ya serikali.
Chama chake tayari kimevunja mazungumzo na serikali ya kutaka kubuni serikali ya muungano ili kumaliza mgogoro unaokumba uchumi wa taifa hilo huku kikiwataka wafuasi wake kuandamana.
Jimbo la Darfur limeshuhudia miaka kumi ya umwagaji damu na rais wa Sudan Omar el Bashir anasakwa na mahakama ya kimataifa ya ICC kwa shtaka la uhalifu wa kivita. CHANZO BBC
0 comments:
Post a Comment