Saturday, 19 July 2014

JOSE MOURINHO ALIANZISHA `ZONGO` NA ASERNAL...AMBWATUKIA JACK WILSHERE!


On the attack: Mourinho has come out on the offensive a month before the new season begins
Mashambulizi yameanza: Mourinho ameanza kuishambulia Asernal kwa maneno ikiwa umebaki mwezi mmoja kuanza kwa msimu mpya.


KOCHA wa Chelsea , Jose Mourinho ameipiga madongo mawili Asernal zikiwa zimesalia siku 29 tu kuanza kwa mitanange ya ligi kuu soka nchini England.
Mreno huyo akizungumza kama  balozi wa BT Sport alidai kiungo aliyemsajili, Cesc Fabregas kamwe hakutaka kurudi Emirates majira ya kiangazi mwaka huu na alisema Jack Wilshere ameonesha mfano mbaya kwa watoto baada ya kukutwa akivuta sigara kwenye Las Vegas wiki iliyopita.
Mourinho alifanikiwa kumsajili Fabregas kutoka klabu ya Barcelona mapema baada ya kuanza majira ya kiangazi, licha ya kuwa Asernal ndio walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuinasa saini ya kiungo huyo.
Kitendo cha Fabregas kujiunga Stamford Bridge kiliwashitua wengi kwasababu nyota huyo alikuwa na mapenzi na washika bunduki na aliwahi kuwa nahodha wao.
Fabregas alionesha kuwa Asernal walimpotezea, lakini Mourinho anadai kiungo huyo kamwe hakutaka kurudi kaskazini mwa London na alisema ilimchukua dakika 20 tu kumsajili.
"Kwa namna gani nilimshawishi? Nilizungumza naye kwa dakika 20," alisema Mourinho.
"Nadhani kiukweli alikuwa anataka kuja hapa. Asernal hawakuwa na jinsi na ndio maana hawakuingilia, lakini sidhani kama alikuwa muwazi kwa hilo. Alikuwa katika uelekeo wetu, kwahiyo ilikuwa rahisi kwangu.
Easy decision: The Chelsea boss claimed it took just 20 minutes to convince Cesc Fabregas to join
Maamuzi rahisi: Kocha wa Chelsea amedai ilimchukua dakika 20 tu kumshawishi Fabregas kujiunga Darajani 

`The Special One` alizungumzia suala la utata la Wilshere kunaswa akivuta sigara wiki hii.
Kiungo huyo wa washika bunduki alipigwa picha akivuta sigara na kuonesha tabia mbaya wakati wa likizo yake.
Ilikuwa mara ya pili katika miezi tisa, Wilshere kuonekana ana sigara mdomoni, licha ya yeye kujulikana sio mvutaji.
Mourinho alisema kiungo huyo wa England hafanyi kazi yake kama mtu wa kuigwa na jamii baada ya kuendeleza tabia hii. Controversy: The England midfielder was seen smoking a cigar and cigarettes given to him by his brother
"Nini wachezaji wa mpira wanafanya, mamilioni na mamilioni ya watu wanatazama, watoto wengi wanatazama," alisema Bosi huyo wa Blues.
"Mimi sio mtaalamu,, lakini sidhani kama mchezaji anaweza kuathirika kiwango chake kwa kuvuta sigara moja akiwa na marafiki zake majira ya kiangazi wakati hayuko mazoezini".
"Anayeathirika ni mtoto wa nyumbani, anaanza kuwaza kama mchezaji mkubwa anavuta, nami naweza kuvuta, hakuna tatizo".
Bad example: Mourinho also blasted Jack Wilshere who was photographed smoking this week
Mfano mbaya: Mourinho pia alimmbwatukia Jack Wilshere aliyepigwa picha akivuta sigara wiki hii.

0 comments: