Mechi
ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini
(Amajimbos) itachezwa Ijumaa, Julai 18 mwaka huu katika Uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Serengeti Boys ambayo imeingia
moja kwa moja katika raundi ya pili ya michuano hiyo inatarajia kuingia
kambini wiki ijayo kwenye hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, na itacheza mechi
hiyo kuanzia saa 10 kamili jioni.
Amajimbos kama ilivyo Serengeti
Boys imeingia moja katika raundi ya pili pamoja na timu za Angola,
Benin, Botswana, Burkina Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon,
Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco, Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na
Zambia.
Mechi ya marudiano itachezwa
Afrika Kusini kati ya Agosti 1na 3 mwaka huu. Iwapo Serengeti Boys
itafuzu itaingia raundi ya tatu itacheza mechi zake kati ya Septemba 12
na 14 mwaka huu wakati marudiano itakuwa kati ya Septemba 26 na 28 mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment