Mgeni
rasmi Mhe. Peter Toima Kiroya wa pili kushoto mkazi wa Manyara Wilayani
Simanjiro ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma
akiwaongoza vijana wa kimasai kundi la Korianga kuingia kwenye boma kwa
ajili ya kushiriki sherehe ya unywaji wa maziwa ikiwa ni mojawapo ya
hatua ya makuzi kwa vijana jana mkoani Manyara, wapili kulia ni Mke wa
Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya.
Mgeni
rasmi Mhe. Peter Toima ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani
Kigoma akipokea Kiyabuyu cha maziwa kutoka kwa Mkewe Bi. Filomena Toima
Kiroya kama ishara ya kuwaonyesha vijana waliohitimu hatua moja ya
makuzi katika sherehe za unywaji wa maziwa Mkoani Manyara katika Wilaya
ya Simanjiro.
Mmoja wa vijana wa kimasai kundi la Korianga akipokea kibuyu cha maziwa
kutoka kwa mke wake kama ishara kuwa kuanzia sasa anaruhusiwa kunywa
maziwa katika boma lake bila ya kujificha kama alivyokuwa akifanya kabla
ya kuingia katika hatua hiyo ya makuzi kwa vijana wa kimasai.
Bw. Onesmo Toima akinywa maziwa yaliyomo katika kibuyu baada ya kuvuka
hatua ya malezi iitwayo Sporio na kuingia hatua ya Korianga katika
sherehe za unywaji wa maziwa zilizofanyika jana Mkoani Manyara katika
Wilaya ya Simanjiro Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Venerose Mtenga akitoa hotuba wakati wa Sherehe za unywaji
wa maziwa kwa vijana wa kimasai kama hatua mojawapo ya malezi kwa
vijana, kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mhe. Peter Toima Kiroya
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma. Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Venerose Mtenga aliyekaa kulia katika picha ya pamoja na
vijana wa kundi la Korianga, watatu kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo
Mhe. Peter Toima Kiroya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani
Kigoma na wapili kulia ni Mke wa Mgeni rasmi Bi. Filomena Toima Kiroya.
(Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini – WHVUM)
0 comments:
Post a Comment