“PRESS RELEASE” TAREHE 20.06.2014.
- MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
- MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA CHANG’OMBE WAILAYANI CHUNYA AVAMIWA NA KUPORWA VITU MBALIMBALI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI
KATIKA SHULE YA SEKONDARI NZONDAHAKI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JOSHUA
BUKUKU (19) MKAZI WA NZOVWE AMEUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI NA MTU
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOSHUA SAID (17) MKAZI WA SIMIKE.
INADAIWA KUWA MNAMO TAREHE
18.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA UWANJA WA SHULE YA
SEKONDARI ST.MARTS ILIYOKO ENEO LA FOREST MPYA, KATA YA FOREST, TARAFA
YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA ULITOKEA UGOMVI BAINA YA MAREHEMU NA
MTUHUMIWA WAKATI WAKICHEZA MPIRA WA MIGUU NA NDIPO MTUHUMIWA KUMPIGA
JIWE LA KICHWANI NA KUMJERUHI.
MHANGA ALIFARIKI DUNIA MNAMO
TAREHE 19.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:32 JIONI WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA
MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA
ALIKUWA ANASOMA SHULE MOJA NA MAREHEMU NA ALIACHA MASOMO AKIWA KIDATO
CHA TATU MWAKA 2013. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MFANYABIASHARA MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEVEN DAISON (33) MKAZI WA CHANG’OMBE
ALIVAMIWA AKIWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WANNE ANAOWAFAHAMU KWA SURA NA
KUMJERUHI KWA KUMKATA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA
KUPORA VITU MBALIMBALI.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA MWAGALA,
KIJIJI CHA CHANG’OMBE, KATA YA MBUYUNI, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA HAO WALIMJERUHI MHANGA KWA KUMKATA
MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA KUMPORA PESA TSHS
1,800,000/=, SIMU PAMOJA NA VOCHA ZA SIMU ZENYE THAMANI YA
TSHS1,200,000/=.
INADAIWA KUWA, KABLA YA TUKIO
WATU HAO WALIFYATUA RISASI HEWANI NA GANDA MOJA LA RISASI YA S/GUN
LIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MHANGA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.
MSAKO MKALI UNAENDELEA ILI KUWABAINI WATUHUMIWA WA TUKIO HILI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MSAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA LAITON ANYELWISYE (32) MKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
UJAZO WA LITA 5.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
19.06.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA UPENDO, KATA
YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA ALIYETAMBULIKA
KWA JINA LA KADIL KANDAM (22) AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
19.06.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU KATIKA ENEO LA IGAWILO, KATA YA
IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO
HASA WAHAMIAJI HARAMU ILI UPELELEZI UFANYWE DHIDI YAO.
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment