Muangalizi: Jose Mourinho (kulia)
amekuwa akiwatembelea watoto wanaosumbuliwa na njaa pamoja na wagongwa
wa UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi wa Mpango wa Chakula
Duniani.
BOSI wa Chelsea, Jose Mourinho
anadhani chama cha soka nchini England, FA kingetoa faini za mpira wa
miguu anazolipa kwa kuwasaida watu wenye shida kama sehemu ya upendo.
Badala ya kuangalia kombe la dunia
mwaka huu nchini Brazil, Mourinho amewatembelea watoto wanaosumbuliwa na
njaa na wagonjwa wenye virusi vya UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama
balozi wa umoja wa mataifa wa Mpango wa Chakula Dunia.
Mreno huyo alisema anataka kuona mpira
unafanya kazi zaidi kusaidia mpango wa Chakula Duniani (WFP) na
akapendekeza FA itumie faini anazotozwa kuwasaidia watu wenye shida.
"Nitalipa (faini) kwa tabasamu kama hela zinakwenda sehemu sahihi," Aliwaambia ITV wakati wa ziara yake.
'Huo ni uzoefu, kwakweli nimepata
uzoefu,". Alisema kocha huyo mwenye miaka 51 huku akishindwa kuzuia
machozi yaliyokuwa yanamlenga.
"Na aina ya uzoefu ambapo najisikia kidogo".
"Ni machungu, lakini wakati fulani huwa ni nzuri kwa roho".
Mpango wa Chakula Dunia ni shirika kubwa la kimataifa linaloshughulikia balaa la njaa duniani kote.
Mwezi mei, Mourinho alitozwa faini na
FA ya Euro 10,000 kwa maneno yake aliyosema juu ya viongozi wa mechi
baada ya Chelsea kufungwa mabao 2-1 na Sunderland na kujikuta akivunja
rekodi ya kucheza mechi 77 bila kufungwa nyumbani.
Mourinho baada ya kutembelea Afrika amesisitiza faini zinazotozwa ligi kuu zipelekwa kusaidia wenye shida.
0 comments:
Post a Comment