Friday, 20 June 2014

KOMBE LA DUNIA: UCHUNGUZI WA FIFA WAENDELEA DHIDI YA MEXICO KWA UBAGUZI


Mashabiki wa Mexico
Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeanza kuchunguza hatua ya kuiadhibu Mexico, baada ya madai kujitokeza kuwa mashabiki wake walihusika katika matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi yao na Cameroon.
Katika taarifa, FIFA imesema kuwa uchunguzi huo umeanzishwa baada ya matamshi kutolewa kuwa mashabiki wa Mexico walionyesha vitendo na matamshi ya kutiliwa shaka.
Aidha duru kutoka FIFA zimeiambia BBC kuwa wanachunguza ripoti ya matamshi machafu kutoka kwa mashabiki wa timu ya Brazil pamoja na mabango ya kibaguzi wakati wa mechi kati ya Croatia na Russia.
Mwaka jana FIFA ilibuni sheria kali ambapo matamshi ya kibaguzi kutoka kwa shabiki wa soka au mchezaji, yanaweza kuchochea adhabu kali hata kulazimisha timu husika kucheza mechi bila ya mashabiki, kunyanganywa alama, kushushwa daraja au hata kufukuzwa kushiriki mchuano.

0 comments: