KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda, ameibuka na kutangaza kuendeleza mihadhara iliyokatazwa na
kupigwa marufuku na serikali.
Mbali na kutangaza hayo
pia amesema watapigania kurudishwa kwa mitihani ya dini ambayo serikali imefuta
mitihani hiyo.
Hayo ameyasema juzi
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kwenye kongamano la
kujadili mada mbalimbali yakiwemo ya mambo yawahusuyo Waislamu nchini
Wakati akitangaza hayo alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani azingatie kauli hiyo kwani ni muhimu waendeleze na kudai hiyo si haki na hiyo ni sawa na kukubali ujinga.
Hivyo alisema mihadhara hiyo itaendelea kama kawaida na atakayejitokeza kukataza mihadahara hiyo watakabiliana nae kwa nguvu zote,” alisema Ponda.

Pia sakata la kufutwa kwa mitihani ya masomo ya dini limeonekena kuwa utata katika kongamano hilo kwani imeonekana kitendo hicho ni kufanya wanafunzi kukosa moyo kujifunza masomo hayo
Hilo limekuja baada ya
serikali kufuta mitihani ya masomo ya dini na kuhakikisha kujifunza pekee
mashuleni
Hivyo waislamu hao
wamesema watahakikisha mitihani hiyo itarudisha kama kawaida kwani wameona
kitendo hicho ni kuua elimu ya dini kwa watoto wa kiislamu
Shekhe hivi sasa anatumikia kifungo cha nje alichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kupatikana na makosa ya uchochezi
Shekhe hivi sasa anatumikia kifungo cha nje alichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kupatikana na makosa ya uchochezi
0 comments:
Post a Comment