MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), Absalom Kibanda anatarajia kuwasili leo akitokea nchini Afrika Kusini
alipokuwa akitibiwa tangu Machi 6, baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na
watu wasiofahamika usiku wa Machi 5.
Katika
taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena,
Kibanda atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo saa 7
mchana na atazungumza na waandishi wa habari.
Kutokana
na ujio huo, Meena aliwaomba wahariri na waandishi kufika uwanjani hapo kuanzia
majira ya saa 6.00 mchana kwa ajili ya kumpokea mwenzao huyo aliyekaa nje ya
nchi kwa miezi mitatu.
“Mwenzetu
kakaa Afrika Kusini kwa siku 90, hii ni fursa nyingine adhimu ya waandishi wa
habari nchini kuonyesha mshikamano na umoja wetu kwa kwenda kumpokea,” alisema.
Kibanda
ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, kuumizwa kwake
kuliitikisa tasnia ya habari nchini na kuzua mijadala mbalimbali ndani na nje
ya nchi.
0 comments:
Post a Comment