BEKI
wa kushoto wa Italia, Mattia De Sciglio ameondolewa kwenye mchezo wa
ufunguzi wa Kundi D dhidi ya England mjini Manaus kesho kutokana na kuwa
majeruhi.
Habari hizo ni pogo kwa kocha wa Azzurri, Cesare Prandelli kwa kikosi chake wakati kesho anaanza kampeni za Kombe la Dunia.
beki
huyo wa AC Milan mwenye umri wa miaka 21, aliumia misuli jana mazoeini
na kupelekwa hospital kwa ajili ya kuanyiwa vipimo vya MRI ili kujua
ukubwa wa tatizo lake.
"Beki
Mattia De Sciglio, baada ya mazoezi leo (jana) huko Portobello
(Mangaritiba), ameumia misuli ya mguu wake wa kushoto,"amesema daktari
wa Italia, Enrico Castellacci.
Prandelli
anatarajiwa kuziba pengo la De Sciglio kwa kumpanga beki wa Inter
Milan, Andrea Ranocchia ni mchezaji wa akina kwenye Fainali hizi za
Brazil.
The
Azzurri inaweza kubadilisha wachezaji kikosini make kutoka orodha ya
awali iliyowasilisha kwa ajili ya michuano hiyo saa 24 kabla ya kucheza
mechi yao ya kwanza.
De Sciglio ameondolewa kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D lakini anatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo na Costa Rica Juni 20.
0 comments:
Post a Comment