Na Mwandishi Wetu
Promosheni
ya Kwea Pipa na televisheni ya Taifa ya TBC kwa kushirikiana na
kampuni ya Push Mobile Media Limited imezidi kupamba moto baada ya
mshindi mmoja zaidi kupatikana.
Deocary
Mkenda ambaye ni mkazi wa Sinza ameungana na wenzake wawili ambao
wamekwisha zawadiwa tiketi zao na sasa kampuni ya Push Mobile Media
Limited inawatafutia pasipoti kwa ajili ya kusafri na kuona mechi ya
Brazil na Cameroon Juni 23 mjini Rio de Janeiro.
Mkenda
(35) ambaye ni Mhasibu katika kampuni ya Ernst & Young ya jijini
anaungana na Donald Milinde Shija (34) mkazi wa Mabibo jijini ambaye ni
mfanyakazi wa kampuni ya Davis and Shirtliff na mshindi mwingine ni
Shaban Athumani Saidi (22) mkazi wa Banana-Kitunda.
Meneja
kampeni wa promosheni hiyo ya Semu Bandora alisema kuwa bado tiketi
mbili kwa ajili ya mashabiki wa soka nchini ili kujishindia tiketi kwa
ajili ya kuona kombe hilo.
Bandora
alisema kuwa droo nyingine itafanyika wiki ijayo na lengo ni kuona
mashabiki wanapata fursa hiyo ya kuona mashindano hayo makubwa kabisa ya
soka duniani.
“Tunawaomba
mashabiki wa soka kuendelea kushiriki katika promosheni hii ili kupata
nafasi ya kuwaona mastaa wa dunia kama akina Benoit Assou-Ekotto, Alex
Song na Samuel Eto’o na yule wa Brazil kama vile Neymar da Silva Santos
Júnior, Thiago Silva, Dan Alves na wengine wengi,” alisema Bandora.
Alisema
kuwa mbali ya tiketi za kombe la dunia, pia kuna zawadi za ving’amuzi
zaidi ya 250, televisheni za flat screen sita na fedha taslimu ambazo
zote zimeandaliwa kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wa soka.
0 comments:
Post a Comment