KIKOSI
cha Cameroon leo kimegoma kupanda ndege kwenda Brazil kwa ajili ya
Kombe la Dunia ili kushinikiza malipo ya posho za kushiriki michuano
hiyo.
Timu
hiyo imebaki katika hoteli yao mjini Yaounde, wakati Waandishi wa
Habari walikuwa nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Cameroon kupata
maelezo juu ya sakata hilo.
Ndege
ilitarajiwa kuondoka Yaounde Saa 3:00 asubuhi kwenda Brazil, wakati
Cameroon inacheza mechi yake ya ufunguzi Ijumaa na Mexico.
Wachezaji
wa Cameroon wiki iliyopita walitaka kugoma hadi kwanza wapewe posh zao,
lakini wakasitisha mgomo huo na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Ujerumani Jumapili iliyopita, liliripotia gazeti la L'Equipe la
Ufaransa.
Cameroon ipo Kundi A na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
0 comments:
Post a Comment