Tuesday, 17 June 2014

KOMBELA DUNIA: MATUMAINI YA WAAFRIKA KTK KOMBE LA DUNIA YAPOTEA BAADA YA ALGERIA KUTAFUNWA NA UBELGIJI 2-1




AFRIKA imeendeleza unyonge katika Kombe la Dunia, baada ya Algeria kufungwa mabao 2-1 na Ubelgiji jioni hii Uwanja wa Mineirao, mjini Belo Horizonte, Minas Gerais, Brazil katika mchezo wa Kundi H.
Algeria watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kulinda bao lao walilolipata mapema kipindi cha kwanza kupitia Sofiane Feghouli aliyefunga kwa penalti dakika ya 25.
Algeria waliiruhusu Ubelgiji kusawasisha kupitia kwa Marouane Fellaini dakika ya 70 na Dries Mertens akafunga la ushindi dakika ya 80.
La kusawazisha; Fellaini kulia akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Ubelgiji bao la kwanza

Algeria pamoja na kufungwa walicheza vizuri na kuibana Ubelgii iliyotumia wachezaji wake nyota wanaotamba Ligi Kuu ya England, Fellaini, Edin Hazard na Romelu Lukaku.
Kikosi cha Ubelgiji kilikuwa: Courtois, Alderweireld, Kompany, Van Buyten, Vertonghen, Witsel, Dembele/Fellaini dk65, Chadli/Mertens dk46, De Bruyne, Hazard na Lukaku/Origi dk58.
Algeria: M'Bolhi, Halliche, Bougherra, Medjani/Ghilas dk84, Ghoulam, Bentaleb, Mostefa, Taider, Mahrez/Lacen dk71, Soudani/Slimani dk66 na Feghoul

0 comments: