Friday, 20 June 2014

KIONGOZI WA MADHEHEBU YA SHIA ATAKA SERIKALI MPYA URAQ



Ali al-Sistani
Kiongozi wa madhehebu ya Shia nchini Iraq Ayatollah Ali al-Sistani ametaka kuundwa haraka kwa serikali mpya.
Katika taarifa iliyosomwa kwa niaba yake, Ayatollah amesema kuwa serikali yoyote mpya ni lazima itoe huduma sawa kwa wanachi wote wa Iraq.
Wapiganaji wa ISIS wamekuwa wakiendesha harakati zao na kutenda unyama wa kutisha
Hata hivyo huenda wengi wakachukulia matamshi hayo kama shutuma kwa waziri mkuu nchini Iraq Nouri al- Maliki.
Wakati huo huo hatma ya kituo kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini Iraq haijulikani wakati mapigano yakiwa yanaendelea kati ya wapiganaji wa Sunni wanaongozwa na kundi la ISIS na vikosi vya serikali.

0 comments: