M/W Makete Bi, Josephine Matiro
.................................................................................................
Mkuu wa wilaya ya makete amewasa viongozi wa kisiasa kuanzia ngazi za vijiji,kata,na tarafa na kutoka
wilaya zinazo zunguka hifadhi za Kitulo, Eneo tengefu la Kipengere na Hifadhi ya
Mlima Rungwe kuwaelimisha wananchi wao umuhimu wa hifadhi hizo badala ya
kuendelea kulumbana juu ya mipaka ya harali ya hifadhi na mashamba ya
wananchi.
Wito huo mumetolewa hivi
karibuni na Mkuu huyo wa wilaya wakati akifungua warsha hiyo kwa viongozi wa
kata amabo ni madiwani na maafisa watenaji,na tarafa pia na wataalamu wanao
simamamia hifadhi hizo zinazo zunguka hifadhi hizo iliyofanyika katika Ukumbi wa
FEMA unao milikiwa na kanisa KKKT Dayosisi Kusini Magharibi usharika wa Matamba
wilayani Makete.
Mkuu huyo wa wilaya alisema
kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuwa ahidi
wananchi kwamba maeneo yalichukuliwa na hifadhi jizo yatarudishwa kwa wananchi
kitu apacho hakipo na hakiwezekani kwani meneo hayo yametengegwa kwa mujibu wa
sheria pia ni agizo kutoka kwa Rais hivyo hakuna kiongozi ambaye anaweza
kutengea agizo hilo.
Alisema kuwa ni wakati sasa
kwa viongozi hao wa siasa wakiwemo madiwani na wabunge wanatoka katika maeneo ya
hifadhi na tengefu kutoa elimu kwa wananchi faida zitokana nazo na umuhimu wa
hifadhi hizo kwa jamii hiyo inayo zunguka badala ya kuendelea
kulumbana na wataalamu walioajiliwa na serikali kwa ajili ya kusimammia hifadhi
hizo.
“Ndugu zangu vingozi wa kata
na tarafa pamoja na hasa nyie madiwani msiwadanganye wananchi kwamba eti maeneo
yaliyo tengwa yanaweza kurudishwa hilo halipo kwani ni hifadhi chache ambazo
wananchi wake wanarusiwa kufanya shughuli zao ndani ya hifadhi lakini hapa kwetu
hakuna kitu kama hicho kwa hiyo mkawambia wananchi hilo haliwezekana,pia tumienu
mikutano ya hadhara ya kuwaleza wananchi faida zitokano uwepo wa
hifadhi hizo” alisema Matiro
Alisema kuwa sehemu nyingi
alizo pita na kusilikiza malalamiko ya wananchi wengi hawaja
elezwa ukweli na elimu ya kutosha juu faida za kuifadhi mazingira na uwepo wa
hifadhi hivyo amewataka viongozi hao kwenda kuwa elimisha wananchi ili kujenga
mahusinano mazuri katika hifadhi na wananchi wano zunguka maneo hayo.
Kwa upande
wake Mwakilishi wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa
Duniani (UNDP) kupitia mratibu mradi
wa kuboresha Mtandao maeneo yaliyo hifadhiwa kusini mwa Tanzania (SPANETS)
Godwell Ole Meing’ataki ambao miongoni mwa waaandaaji wa warsha
hiyo alisema kuwa lengo la kuwaita viongozi hao wa kisiasa ni kutaka kujadili
kwa pamoja na kuondoa migogoro ambayo kimsingi haina tija kwa taifa.
Alisema sababu nyingine ya
kufanya warsha hiyo kujadili kwa pamoja na viongozi hao ilikuibua miradi
itakayo nufaisha wananchi wanao zunguka katika hifadhi hizo kama
jamii zingine ambazo zipo karibu na maeneo ya hifadhi zinavyo nufaika.
Alisema kuwa hifadhi ya za
Kitulo,Kipengere, na Mlima Rungwe ni hifadhi tegemezi na haziwezi kujiendesha
zenyewe na zinategemea bajeti kutoka hifadhi zingine hivyo
wameamua kuitisha warsha kuyatangaza maeneo hayo kiutalii ili yaweze kujitegemea
na hatimaye yaweze kuwahudumia wana jamii wanao zunguka maeneo hayo.
Godwell alisema kuwa elimu
inahitajika kwa jamii na nguvu zinahitajika kwa kutangaza vivutio vya utalii
hasa kwa ukanda huu wa nyanda kusini ambako inaonekana haujaeleweka kikamililifu
ili kuweza kuongeza kipata kwa jamii na hifadhi zenyewe.
Kwa upande wake mhifadhi
Mkuu wa Mbuga kitulo Deus Mzimba ambao ndo wenyeji ni waandaaji wa warsha hiyo
alisema kuwa vingozi wa kisiasa kuanzia wenyeviti wa vitongoji,vijiji,wakitumiwa
wanaweza kupepusha migogro hiyo kwana imekuwa ikinzia ngazi ya vitongoji.
Mbali na hilo Mzimba alisema serikali kwa
kushirikana na vingozi hao wana wajibu kutoa elimu ya ujasilimali kwa wananchi
wanao zunguka maeneo hao ili wanapo kuja watalii waweze kupata huduma kwa
urahisi.
Warsha hiyo ilianza jana na
ilitajiwa kumalizika leo ikiwa imefanyika kwa siku mbili washiriki wa warsha
hiyo ni madiwani,watendaji wa kata,na makatibu tarafa kutoka wilaya
Makete,Njombe kwa Mkoa wa Njombe na Halmashauri za Mbeya Rungwe na Busokelo
kutoka Mkoa wa Mbeya na watalaamu wa hifadhi kuoka Mlima Rungwe, Kitulo na
Kipengele amapo wanatarajiwa kutoka na maazimio,na mapendekezo ya pamoja ili
kuondokana na migogoro inayotokea katika hifadhi hizo.
Mwisho.
....................................................................
Na Esther Macha, mbeya
0 comments:
Post a Comment