Wednesday 4 November 2015

Wema Sepetu Amtusi Diamond Baada Ya Kununua Gari La Milioni 200 ( Range Rover )



Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ameangusha bethidei baab’kubwa ambayo imesheheni kufuru ya aina yake na ‘kumtusi’ hadharani mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kumsema kuwa ni mtu wa kununua magari ya bei rahisi hivyo hawezi kuifikia hadhi yake.

Sherehe hiyo iliyosheheni mastaa kibao Bongo, ilifanyika katika ukumbi wa Wema Sepetu uliopo ndani ya jengo la Millenium Towers, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanadadahuyo alizua gumzo la aina yake baada ya kujizawadia gari aina ya Range Rover lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.

Ulipofika wakati wa zawadi, mastaa na waalikwa mbalimbali walishindana kumtunza mrembo huyo asiyechuja Bongo, vitu mbaimbali vya thamani, zikiwemo fedha taslimu ambapo ‘wekundu wa Msimbazi’ walionekana kutapakaa katika eneo maalum la kupokelea zawadi alilokaa Madam.

Alivyomtusi Diamond
Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la zawadi ndani ya ukumbi, ndipo Wema alipowatoa nje waalikwa na kuwaonyesha gari lake jipya aina ya Range Rover ambalo linasadikika kuwa litakuwa la kwanza kumilikiwa na msanii wa kitanzania kutokana na thamani yake.

“This is my new brand car, yaani ni mpya ya mwaka 2015, hakuna kenge yeyote anayeweza kufuata nyendo zangu na yule ambaye alikuwa akijigamba eti alinipa zawadi ya gari la elfu 30, nini na nini na hili aseme sasa maana mimi si wa kuhongwa kila kitu,” alisema mrembo huyo, kauli iliyoonyesha wazi kumlenga Diamond, ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari lenye thamani ya shilingi milioni 30 miaka michache iliyopita.

Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mwanamuziki Queen Darleen, Diamond Plutnumz amzawadia gari mpya

 
Leo star na mkongwe wa Bongo Flava aitwae Queen Darleen, anasheherekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
 
 
Sasa kaka yake ambaye pia ni Icon wa Muziki Afrika hivi sasa Naseeb ‘Diamond’ Abdul, ameamua kumzawadia zawadi ya gari mpya dada yake.

kupitia ukurasa wake wa Instagram, Plutnumz ameweka picha ya gari hiyo na kuandika ‘Happy Birthday my luvly and beutiful sisy.. let dat small gift be your bornday memory from your young brother… “

0 comments: