Wednesday 6 August 2014

HOWARD WEB ASTAFU RASMI KUPIGA VIRIMBI , SASA BOSI WA MAREFA


REFA maarufu England, Howard Webb amestaafu kupuliza kipyenga baada ya miaka 25-na sasa atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya marefa (PGMOL).
Refa huyo mwenye heshima kubwa amechezesha mechi zaidi ya 500 za Ligi Kuu ya England na nyingine za mashindano ya soika nchini humo tangu apande daraja mwaka 2003.
Webb pia amechezesha fainali mbili za Kombe la Dunia na mbili za Kombe la Mataifa ya Ulaya, kabla ya kuweka rekodi ya kuwa refa wa kwanza kucheza fainaliEURO na Kombe la Dunia kwa mwaka mmoja, 2010.

Ametungika kipyenga: Howard Webb amehitimisha maisha yake ya urefa 
Top level: Webb, seen here with Manchester United striker Wayne Rooney, has taken charge of more than 500 matches in the Premier League and Football League since becoming a Select Group official in 2003
kashfa moja kubwa ya Webb enzi zake ilikuwa ni kuibeba Manchester United, hapa anazungumza na mshambuliaji wa timu hiyo, WAYNE ROONEY katika moja ya mechi alizochezesha

0 comments: