Watoto
wa Shule ya Msingi Kanindi na Shule ya Msingi Majimoto Tarafa ya Mamba
Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Wakati wa maandamano kusherehekea siku ya
mtoto wa Afrika yaliyofanyika kijiji cha Majimoto wilayani mlele
Mkoani Katavi huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali
kupinga ukatili dhidi ya watoto.
………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewaasa wazazi Mkoani katavi kuwa na uchungu wa elimu ili kuleta chachu ya mabadiliko katika jamii. .Dkt Rutengwe alitoa ushauri huo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga kwenye sherehe za maazimsho ya siku ya mtoto wa Afrika mazimisho yaliyoazimishwa kwenye Kijiji cha Majimoto Kata ya Maji moto Wilayani Mlele kimkoa. Amewashauri wazazi kuwathamini, kuwalinde na kutowatendea ukatili wa aina yeyote watoto kwani kuwatendea ukatili ni kosa kisheria
Akifafanunua zaidi Dkt Rutengwe alisema wazazi lazima waone uchungu wa kusomesha watoto, wawe na uchungu wa kujitoa kuwapa haki ya elimu, haki ya kulindwa na kuthamini hivyo wazazi lazima wajitoe katika kuchangia elimu ya watoto wao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamewatendea haki watoto.
Iwapo watafanya hivyo watoto watapata elimu inayositahili na ni haki yao ya kumsingi kuwasomesha watoto huwezi kuzaa mtoto usimpatie elimu utakuwa hujamtendea haki. .Akaongeza kuwa wazazi lazima wawe makini katika kuwasimamia watoto, kuwalinda kuwatunza na kuwathamini na hiyo ni haki ya mtoto, na kuongeza kuwa watoto nao wanao wajibu wa kuwaheshimu wazazi na wale wote wanaowazidi nao ni wajibu huo pia. Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiongea katika mazimisho hayo alieleza kuwa sehemu kubwa ya watu katika mkoa wa Katavi ni watoto na vijana.
Mhandisi Kalobelo akaongeza kuwa kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 takwimu zinaonesha kuwa katika Mkoa wa Katavi yenye idadi ya watu wapatao 564,000 kati yao watoto wa kuanzia umri wa miaka 0 hadi miaka 14 wapo 280,000 na vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35 wapi 180,000 hali inayoonesha kuwa watoto na vjiana wapo asilimia 83. “Kutokana na hali hiyo wanakatavi wasipopata elimu tutakuwa tumekosa kuwatendea haki watoto wetu”alisema Mhandisi Kalobelo. Akasema kuwa haki ya mtoto ni kupendwa,kusomeshwa na kupata elimu bila vikwazo pia nao watoto wana wajibu wa kuwa na heshima na kusoma kwa bidii. Akawaasa waache uvivu wasome kwa bidii ili baadae waje kuwa viongozi wa kuongoza kuanzia kwenye Kijiji,Kata,Tarafa Wilaya Mkoa na Taifa kwa ujumla yote hayo yatapatikana kwa kusoma kwa bidii na kupata elimu. Kwa upande wao watoto katika risala yao walieleza ukatili wanaofanyia maeneo mbalimbali kuwani pamoja na kunyanyaswa, kunyimwa haki ya elimu,chakula, kupigwa, ajira kwa watoto,kuozeshwa wakiwa na umri mdogo,kuozwa, pamoja na mateso ya kila aina, ambapo takwimu zinaonesha kuwa akina mama waongoza kwa kuwafanyia watoto hasa majumbani” Kauli mbiu ya mwaka huu ni kupta elimu bora na isiyo na vikwazo ni haki ya kila mtoto”.
Na Kibada Kibada –Katavi
0 comments:
Post a Comment