MAGAZETI YACHARUKA: ‘ENGLAND NI ‘WAJINGA’ WA KOMBE LA DUNIA!’
WAKATI FA, Chama cha Soka England,
kikithibitisha kuwa Meneja wao Roy Hodgson atabakia kazini licha ya
kupigwa chini huko Brazil, Staa wa England Wayne Rooney amewaomba radhi
Mashabiki kwa kushindwa kwao lakini Magazeti ya Nchini humo yamecharuka
na kuwashambulia FA na Meneja wao.
SOMA ZAIDI:
ROONEY AOMBA RADHI
Wayne
Rooney amewaomba radhi Mashabiki kwa England kutolewa nje ya Fainali za
Kombe la Dunia huko Brazil huku wakiwa wamebakisha Mechi moja ya Kundi
D.
Ijumaa, Costa Rica iliifunga Italy Bao
1-0 katika Mechi ya Kundi D na Matokeo hayo kuthibitisha England ipo nje
ya Mashindano hayo na hiyo ni mara ya kwanza tangu Mwaka 1958 kwa
England kushindwa kufuzu kuingia Raundi ya Pili.
Mwaka huo 1958, England ilitoka Sare Mechi zao zote 3 za Makundi ikiwa ni pamoja na Brazil iliyotwaa Ubingwa.
Akiposti kwenye Ukurasa wake wa Facebook, Rooney alisema kutolewa huko kumewaumiza sana.
Alieleza wao walikuwa na matumaini makubwa lakini bahati mbaya mambo hayakwenda vizuri na akawaomba radhi Mashabiki wote.
FA YATHIBITISHA HODGSON KUBAKI MENEJA!
Roy Hodgson atabakia kazini kama Meneja wa England hadi mwisho wa Euro 2016 kwa mujibu wa Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke.
Uamuzi huo umekuja licha ya England
kutolewa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil baada ya Mechi 2
tu za Kundi D walizofungwa 2-1 na Italy na pia Uruguay kwa Mabao hayo
hayo.
MAGAZETI YACHARUKA: ‘ENGLAND NI ‘WAJINGA’ WA KOMBE LA DUNIA!’
Lakini Magazeti ya huko Uingereza
yamekuja juu na kudai ‘England imebakishwa kama Mjinga anaechekelea
kualikwa Pati’ wakati jingine lilisema ni ‘matusi’ kwao kumtangaza
Hodgson kwamba yuko salama kwenye kazi yake ya Umeneja.
Gazeti la The Daily Telegraph limeitaka FA iwaombe radhi Washabiki wa England.
KOMBE LA DUNIA-Brazil 2014
MSIMAMO:
KUNDI D |
||||||||
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
Costa Rica |
2 |
2 |
0 |
0 |
4 |
1 |
3 |
6 |
Italy |
2 |
1 |
0 |
1 |
2 |
2 |
0 |
3 |
Uruguay |
2 |
1 |
0 |
1 |
3 |
4 |
-1 |
3 |
England |
2 |
0 |
0 |
2 |
2 |
3 |
-1 |
0 |
0 comments:
Post a Comment