Shambulio limetokea katika jimbo la Yobe nchini Nigeria wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia.
Jimbo hilo limewekwa katika hali ya hatari huku
maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio yanayofanywa na
wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitolea mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa katika jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.
Mfanyikazi mmoja wa hospitali ameaimbia BBC kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.
Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za kombe la dunia kutokana na hofu ya Usalama.
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.
Hali ya hatari
Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila mara ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram..Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009
0 comments:
Post a Comment