MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaendelea kujiwinda na msimu
mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara na ligi ya mabingwa Afrika mwakani.
Kocha
msaidizi wa klabu hiyo, Kalimangonga Ongala amesema lengo la kuanza mazoezi
mapema ni kusuka kikosi chao kwani wanajua kazi iliyopo mbele yao ni kubwa.
“Tunahitaji
kutetea ubingwa wetu, tunahitaji kufanya maandalizi mazuri ya ligi ya mabingwa
Afrika. Kwa majukumu haya makubwa, tumeamua kuanza mazoezi mapema”.
“Tulianza
na wachezaji kama 12 tu, wengine hawajafika. Kuna wachezaji wapo na timu ya
taifa na wale `Maproo` wengi hawajafika bado. Kwasasa tunafanya mazoezi mepesi
ya kupasha misuli tu, siku chache tutaanza mazoezi mazito rasmi”
“Kocha
anatarajia kuja wiki hii, nadhani atakuja na program nzima ya mazoezi”. Alisema
Ongala.
Mazoezi
hayo ya Azam fc leo yanaenda siku ya tatu tangu kuanza ikiwa ni pamoja na
kuongezeka kwa wachezaji.
Wachezaji
ambao wameongezeka katika mazoezi hayo ni Abubakari sure Boy, Agrey Moris,
Aishi Manula, Saidi Molad pamoja na Didier Kavumbagu.
Mazoezi
hayo yanaendelea kwenye uwanja wa Azam comprex uliopo chamazi ambapo kwa sasa
wachezaji wanafanya Mazoezi mepesi mepesi ya kulainisha viungo pamoja na
umiliki wa Mpira.
Kocha
mkuu Mcameroon, Joseph Marios Omog anatarajia kujiunga na kikosi Ijumaa ya wiki
hii.
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment