Xabi Alonso, Kiungo wa Real Madrid, ametangaza kustaafu kuichezea Nchi yake Spain.
Alonso, Miaka 32, amekuwa mmoja wa kiini
cha mafaniko ya Spain iliyotwaa EURO 2008 na EURO 2012 pamoja na Kombe
la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Juzi Alonso aliichezea Spain Mechi yake
ya 112 ilipofungwa 2-0 na Chile kwenye Mechi Kundi B na kutupwa nje ya
Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Kwenye Mechi hiyo, Alonso alibadilishwa wakati wa Mapumziko baada kupwaya na kupokonywa Mpira uliozaa Bao la Kwanza la Chile.
Lakini Alonso ndie Mchezaji pekee
aliewafungia Spain Bao pekee kwenye Mashindano haya huko Brazil
alipofunga kwa Penati kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi B waliponyukwa Bao
5-1 na Netherlands.
Mara baada ya Spain kutupwa nje ya
Fainali ya Kombe la Dunia, Alonso alisema: “Vitu vinabadilika. Zama
zinaisha kwa kufungwa…na hiki kilikuwa kipigo kichungu. Hatukutegemea
lakini ndio mchezo. Hivi vitu vinatokea. Hatukutegemea lakini ni lazima
tuyakabili majonzi yetu vile vile kama tunavyofurahia, kama Wanaume.”
Aliongeza: “Tumecheza dhidi ya Timu
zilizojitayarisha vyema na sasa tunarudi nyumbani. Inauma lakini huu
ndio mpira. Kama nilivyosema, tulijua namna ya kushinda, sasa inabidi
tujue namna ya kushindwa!”
Mbali ya Alonso kutangaza kustaafu pia
kuna wasiwasi kuwa Kiungo Xavi na Kipa Iker Casillas, ambao wote
wamecheza ovyo huko Brazil, wanaweza kufuata nyayo zake.
Zipo habari kuwa Kocha wa Spain, Vicente
del Bosque, hasa kwa vile Shirikisho la Soccer la Spain, RFEF, linaunga
mkono aendelee na kazi yake.
0 comments:
Post a Comment