Sunday 1 June 2014

BAADA YA KUTEMWA, NAVAS AWATAKIA KILA LA KHERI HISPANIA KUTETEA KOMBE LA DUNIA



 Navas wishes Spain good luck after World Cup snub
 Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 12:01 jioni

BAADA ya kuachwa na Vicente del Bosque, Jesus Navas na Daniel Carvajal wamewatakia kila la heri wachezaji wenzao wa timu ya taifa ya Hispania kueleka kutetea ubingwa wao wa kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Navas aliachwa katika kikosi chake na kocha alieleza kuwa sababu ni kutokuwa fiti baada ya kupona majeruhi ya kifundo cha mguu siku za karibuni.
Nyota huyo mwenye miaka 28 akucheza mchezo wa mwisho wa ligi kuu nchini England mwezi aprili, lakini amesema amafurahi sana kwasababu ameimarika.
“Ninajivunia kuimarika kwangu kwa wakati muafaka na nilitegemea kulitetea taifa langu nchini Brazil”. Ameandika Navas katika mtandao wake wa Twita.
“Nawatakia kila la kheri wachezaji wenzangu na kocha wangu mafanikio makubwa katika kutetea ubingwa”.
Naye beki wa Real Madris, Carvajal alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha awali cha wachezaji 30 kabla ya kuachwa katika kikosi cha mwisho.
Beki huyo ametwiti: “ Ni aibu kukosekana katika kikosi cha mwisho, lakini najivunia kwasababu nilikuwa karibu kutajwa. Nawatakia Hispania kila la heri”.
Wakati  huo huo kiungo wa Atletico Madrid, Koke amefurahi kujumuishwa katika kikosi cha Hispania baada ya kufanya vizuri katika michuano ya UEFA na kwenda kushiriki fainali zake za kwanza za kombe la dunia.
“Nimefurahi kuchaguliwa kwenda Brazil, nitakuwa makini kuisaidia timu yangu”.

0 comments: