ARGENTINA
imetinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia, baada ya kuilaza Iran bao
1-0 kwa mbinde jioni hii Uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte,
Brazil.
Shukrani
kwake Nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi aliyefunga bao hilo pekee
dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za
kawaida za mchezo huo, akifumua shuti kutoka umbali wa mita 25.
Messi akijiandaa kufumua shuti lililoipa ushindi Argentina
Ni Mimi; Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Argentina dhidi ya Iran leo
Argentina sasa inatimiza pointi sita baada ya mechi mbili na kusonga mbele, ikiwaachia Iran, Nigeria na Bosnia kibarua cha kuwania nafasi ya pili ya kufuzu kutoka kundi hilo.
Iran
waliibana haswa Argentina katika mchezo wa leo na ilibaki kidogo tu
wafanikiwe kupata sare, sifa zimuendee kipa wao Haghighi aliyeokoa
michomo mingi ya hatari.
Kikosi
cha Argentina kilikuwa: Romero, Fernandez, Garay, Zabaleta, Rojo, Gago,
Mascherano, Di Maria/Biglia dk90, Aguero/Lavezzi dk77, Messi na
Higuain/Palacio dk77.
Iran:
Haghighi,Haji Safi/Haghighi dk88, Hosseini, Sadeghi, Nekounam,
Shojaei/Heydari dk77, Timotian, Montarezi, Ghoochannejad,
Dejagah/Jahanbakhsh dk85 na Pooladi.
0 comments:
Post a Comment