Tuesday 20 May 2014

LIGI KUU VPL KUANZA AGOSTI 24 TIMU 16 KUGOMBEA MWALI

RATIBA ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka Julai 24, mwaka huu na michuano hiyo ya kusaka bingwa wa nchi itaanza mwezi mmoja baadaye, Agosti 24 mwaka huu. Taarifa ya TFF leo, imesema kwamba usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2014/2015) wa ligi hiyo unaanza Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
Mabingwa; Azam FC wataanza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Agosti 24, mwaka huu
Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11 mwaka huu.  Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu. Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu. Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 4 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 5 na 6 mwaka huu. Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka huu). Tayari TFF imesema timu za Ligi Kuu msimu ujao zitaongezeka kutoka 14 za sasa hadi 16, ingawa haijaweka wazi kama juu ya timu zitakazoongezeka kama zitatoka katika zilizoshuka au zilizokosa nafasi ya kupanda katika mfumo wa zamani.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

0 comments: