Tuesday 20 May 2014

COTE D’VOIRE ITAWEZA KUVUNJA REKODI YA “AFRICA GOLDEN GENERATIONS” BRAZIL 2014?



http://www.ghanasoccernet.com/wp-content/uploads/2011/03/didier-drogba-ivory-coast.jpgIvory Coast ni miongoni mwa timu chache kutoka bara la Afrika ambazo zitaliwakilisha bara hili katika Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Algeria, Cameroon, Ghana na Nigeria zimetinga katika kushiriki fainali hizo ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu sio pekee kwa timu zilizopangwa kwenye makundi lakini pia kwa timu zinazotoka bara moja.

Ukilitazama bara la Ulaya utakutana na ushindani usio kifani Ujerumani ikitaka kuweka rekodi safi katika fainali hizo, hali kadhalika kwa Hispania dhidi ya Uholanzi.

Haitoshi Italia itataka kuwapiku Ufaransa hali kadhalika Ureno nayo ikiwania nafasi muhimu katika fainali hizo dhidi ya Uingereza pia Bosnia-Herzegovina.

Bara la Amerika ya Kusini nalo pia linataka kulibakisha Kombe hilo barani humo, kukitarajiwa kuwa na ushindani wa kukata na wembe, Argentina kuonyesha ubabe kwa Brazil, Uruguay dhidi ya Chile.

Hivyo barani Afrika hakuna asiwajua Tembo wa Afrika, jina lao zuri linaongeza ladha kutokana na wazungu wengi kumfahamu Tembo kwa kutalii nchi za Afrika wanakopatikana kwa wingi.
Ivory Coast ambayo kwenye viwango vya soka imeshangaza nchi nyingi hata za barani Ulaya kutokana na usakataji kabumbu wenye ladha ipo katika nafasi 25 za juu kila mwezi inapotangazwa, kwa bara la Afrika imeshika nafasi ya kwanza kwa muda mrefu sasa.

http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Yaya+Toure+Didier+Drogba+Ivory+Coast+v+Tunisia+CrZsbK3Pvxjl.jpgNi muongo mmoja hivi umepita, tangu kizazi cha soka kutoka Jijini Abdijan kilipojitokeza na kupenyeza makucha yake katika soka la kimataifa.

Akademi ya ASEC Mimosas imetoa wakali Emmanuel Ebou, Didier Zokora, Salmon Kalou, Kolo Toure na mdogo wake Yaya Toure isipokuwa Didier Drogba ambaye anawika bila kutoka katika akademi hiyo maarufu.

Ivory Coast inaandika historia nyingine katika Kombe la Dunia ikizama kwa mara ya tatu, mwaka 2006, 2010 na 2014. 

Je, Tembo hao wa Afrika wa sasa, wataweza kuweka rekodi tamu na yenye kuvutia kuzidi vikosi 4 bora ambavyo nimevianisha kutoka bara la Afrika vilivyowahi kufanya mambo makubwa katika ulimwengu wa soka (African Golden Generations)?

KUNDI C BRAZIL 2014
http://www.independent.co.uk/migration_catalog/article5060187.ece/alternates/w620/Kalou.jpeg
Katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil makundi 8 yatachuana kusonga mbele katika hatua ya 16, robo (8) , nusu (4) na fainali (2) ili kulinyakua Kombe hilo ambalo linachezwa kwa mara ya 20 sasa.

Kundi C linaundwa na Colombia, Ugiriki, Ivory Coast na Japan.

Colombia inanolewa na Kocha Jose Pekerman, ambapo rekodi yake nzuri katika Kombe la Dunia ni pale ilipofika hatua ya 16 katika Fainali za Kombe la Dunia 1990.

Mwaka huu linamtegemea aliyezaliwa mfungaji Radamel Falcao ambaye atakuwa bega kwa bega na mchezaji mwenzake wanayesakata kabumbu pamoja katika klabu ya AS Monaco, Javier Rodriguez.

Ugiriki inafundishwa na Fernando Santos, ikiwa na rekodi bora kufika hatua ya makundi 1994 na 2010.

Nchini Brazil, Ugiriki macho na masikio yatakuwa kwa wazoefu wao Georgios Samaras anayechezea klabu ya Celtic akiwa na mkongwe Dimitris Salpingidis katika safu ya ushambuliaji ambao walitoa msaada mkubwa katika mechi za kufuzu.

Japan ipo katika kundi hili chini ya uangalizi wa Kocha Alberto Zaccheroni, ikiwa na rekodi ya kufika hatua ya 16 bora Kombe la Dunia 2002 na 2010.

Samurai watakuwa wakitegemea umahiri wa nyota asiyechuja Keisuke Honda  huku Shinji Kagawa naye akitarajiwa kutoa msaada wa karibu kuhakikisha wanafikia malengo, licha ya maneno mengi wakati wakiwa kwenye harakati za kufuzu.

Ivory Coast inanolewa na Sabri Lamouchi ambaye alipokea kazi kutoka kwa Valid Halidhozic anayeinoa Algeria. Tembo hao rekodi yao bora ni ile walipofika hatua ya makundi katika fainali za Kombe la Dunia 2006 na 2010.

Safari hii, Yaya Toure mchezaji bora barani Afrika 2013 na Kiungo mahiri Ligi Kuu England msimu 2013/2014 ndiye anayekodolewa macho kutokana na aina yake ya usakataji soka ulio makini.

Hata hivyo hatakuwa peke yake atakuwa na watalaamu wengine ambao wameisaidia sana timu hiyo katika michuano mbalimbali ya kimataifa Didier Drogba, Salmon Kalou na Wilfred Bony.

4 AFRICAN GOLDEN GENERATIONS
 http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Yaya+Toure+Didier+Drogba+Belgium+v+Ivory+Coast+gUJHMSFUrnUl.jpg
Ivory Coast inaingia katika wakati mgumu wa kuhakikisha ubora wao kwa vikosi vifuatavyo vilivyowahi kufanya makubwa barani Afrika kwa takribani miongo miwili.
  1. MISRI 2006-2010
Mpaka sasa hakuna taifa lolote barani Afrika lililochukua Kombe la Mataifa ya Afrika mara tatu (hat trick) mfululizo kati ya mwaka 2006 hadi 2010 isipokuwa ni Misri.
Misri ilifanya hivyo mwaka 2006, 2008 na 2010; hata hivyo kulingana na ushindani mkubwa katika soka kwa sasa inaonyesha wazi kuwa hakuna taifa litakalofanya hivyo katika miaka ya karibuni.
Wachezaji wa kizazi hicho; Wael Gomaa na Essam El-Haddary walikuwepo wakati Mafarao wakifanya kazi ya ziada, Ahmed Hassan, Hossam Hassan, Mohamed Aboutrika, Emad Moteab, Amr Zaki, Gedo na Mido walitoa mchango mkubwa.
Wachezaji hao wakati wakifanya hayo walio wengi walitoka katika klabu ya Al Ahly.
Licha ya kuonyesha rekodi safi Misri ilishindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014 kutokana na mapinduzi ya kisiasa nchini humo, kabla ya hapo walikosa WOZA 2010 na kuwapa nafasi Cote d’Voire na Cameroon kutinga katika fainali hizo.
  1. NIGERIA 1994-1998
Katikati ya miaka ya 1990; Nigeria ilikuwa inatisha katika soka barani Afrika ambapo haikuchukua muda mwaka 1994 waliandika historia ya kutinga Kombe la Dunia nchini Marekani.
Hata hivyo Nigeria ambao walijikuta katika kikwazo kikubwa wakipangiwa na Argentina walishindwa kufurukuta na kujikuta wakiishia hatua ya 16 bora.
Mwaka 1996 walifanya marekebisho makubwa na wakatwaa Medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki ya Atlanta.
Kutwaa medali kwa Super Eagles kuliwatia wehu, ndipo wakatinga katika fainali za Kombe la Dunia 1998 nchini Ufaransa na kwa kuonyesha wako vizuri, waliwazabua Hispania (La Fuja Roja) katika mechi ya ufunguzi.
Utawakumbuka wachezaji walioiwakilisha vizuri Nigeria miaka hiyo, Sunday Oliseh, Taribo West, Finidi George, Jay Jay Okocha, Nwako Kanu na wengineo.
Ikilinganishwa, Ivory Coast ya sasa ipo tofauti kabisa na Super Eagles ya wakati huo; kutokana na wachezaji wake wengi kutokuwa na majina makubwa katika vilabu walivyokuwa wakichezea.
  1. CAMEROON 2000-2003
Simba wasioshindika “Indomitable Lions” walikuwa imara sana miaka ya 1980 hadi 1990 wakichukua mataji mawili ya AFCON na kuishia hatua ya robo fainali nchini Italia.
Miaka 10 baadaye, kilizaliwa kizazi ambacho ni Kizazi cha Dhahabu, mwanzoni mwa karne ya 21, Cameroon ilikuwa haikamatiki (unstoppable), wakitwaa AFCON 2000, miezi michache baadaye walitwaa Medali ya Dhahabu Olimpiki nchini Australia.
Mwaka 2002, “Indomitable Lions” waliweka rekodi ya kwanza kuitungua Senegali kwa penati mjini Bamako, nchini Mali tangu walipofanya hivyo 1965.
Hata hivyo, mwaka 2003 walikumbwa na simanzi ya kuondokewa na nyota wao waliyetengeneza kizazi cha dhahabu, Injini ya Cameroon Mac-Vivien Foe alipoanguka katika Uwanja wa Stade Gerland na kufa papo hapo.
Pierre Wome atakumbukwa sana akiikosesha bahati Cameroon kufuzu Kombe la Dunia 2006 wakati huo wakitokea kwenye machungu ya kuishia hatua ya robo fainali AFCON.
  1. GHANA 2009
Wakitokea katika U-20 (Black Satellites), waliweka historia kwa bara la Afrika kwa kizazi cha dhahabu, wakitwaa Kombe la Dunia U-20 nchini Misri.
Kocha Milovan Rajevac aliwaona nyota Daniel Adjei, Samuel Inkoom, Jonathan, David Addy, Emmanuel Agyemang-Badu, Andrew Ayew, Daniel Opare na Mohammed Rabiu na kuwaingiza katika kikosi cha Black Stars.
Kikosi hicho ndicho kilisababisha Ghana ikang’ara katika fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini wakiishia robo fainali, wakikosa mkwaju wa penati dhidi ya Uruguay ambao Luis Suarez aliokoa kwa mikono na kuwanyima kutinga hatua ya nusu fainali.

Yaya Toure(31) anaichezea Klabu ya Manchester City ambayo imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2013/2014 ikiwa ni taji la pili ndani ya miaka mitatu huku nyota huyo akitupia mabao 20 katika Ligi Kuu nchini England.
 http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2010/06/15/article-1286893-0A0C1300000005DC-254_468x378.jpg
Yaya ameichezea Ivory Coast mechi 86 tangu mwaka 2004 na akifumania nyavu mara 16
Salmon Kalou(28), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea sasa yupo Lille LOSC amechezea Ivory Coast mechi 64 akitupia mabao 23.

Nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba (36), akiicheza na Galatasaray ya nchini Uturuki ambapo vilabu vingine vipo mbioni kutaka saini ya yake baada ya Kombe la Dunia ameichezea Ivory Coast mechi 99 akizifumania nyavu mara 63.
http://ghanasoccernet.com/wp-content/uploads/2014/01/Ivory-Coas.jpg
Mchezaji wa siku nyingi wa Tembo wa Afrika, Didier Zokora (33) aliyeichezea Ivory Coast na kuvunja rekodi ya kucheza mechi 118 na kutupia bao moja akisaidiwa na Gervinho (AS Roma), Cheki Tiote (Newcastle), Wilfred Bony (Swansea) na wengineo wataweza kuvipita vikosi hivyo vya dhahabu nilivyokuanishia hapo?

0 comments: