Tuesday 20 May 2014

CHATU MDOGO AKAMATWA JIJINI MBEYA...... BAADA YA JUHUDI KUBWA KUFANYIKA



Mganga wa Jadi Mazoea Hamisi(30) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani(Kushoto) na msaidizi wake Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya wakimwonesha chatu waliyemkamata HATIMAYE juhudi za kumsaka nyoka mkubwa aina ya Chatu anayesadikiwa kuwepo maeneo ya pembezoni mwa mto Meta jijini Mbeya zimeanza kuzaa matunda baada ya Chatu mdogo anayesadikiwa kuwa mtoto kukamatwa. 
 
Juhudi za kuanza kumsaka nyoka huyo zilianza siku chache baada ya mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kutoa taarifa ya tahadhari kwa wakazi juu ya uwepo wa nyoka huyo mkubwa katika eneo hilo na kuwataka wakazi kuwa makini wanapopita katika njia za mkato zilizopo kwenye maeneo anayotajwa kuonekana. 
 
Wataalamu ambao ni waganga wa jadi wakishirikiana na maafisa maliasili kutoka halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamefanikiwa kumnasa chatu mdogo anayesadikiwa kuwa ni mtoto wa chatu ambaye amekuwa akionekana. 
 
Wataalamu hao wakiongozwa na Mazoea Hamisi(30) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani wameweza kumnasa chatu mdogo waliyemkuta pembezoni mwa Mto Meta jirani na hoteli ya Rift Valley. 
 
Alisema baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini kwa bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo alipofanikiwa kumkamata. 
 
Kwa mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya mkoani hapa, Chatu aliyekamatwa ni mdogo na juhudi za kuendelea kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo. 
 
Alisema mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie. 
 

0 comments: