Iyena iyena....... Risala kwa mgeni rasmi kutoka kwa vijana wa UVCCM tawi la Kagera Car wash. Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa, aliwakabidhi wanawak wajasiliamali kiasi cha Tsh.100,000/= baada ya kusema kuwa wanao mfuko wao wa Tsh.300,000. Vijana waliahidiwa Jozi moja ya Jezi na kwamba waandike barua ili wasaidiwe mambo ya kuwakomboa kiujasiliamali ingawa walisema kuwa wanahitaji mashine ya kuoshea magari. Mbunge, Dr. Mary Mwanjelwa, hakutoka bure eneo la Kagera, alipewa zawadi ya chungu cha maua na kinyago. Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr.Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wanachama wa CCM eneo la Kagera Car wash Jijini Mbeya na baadae alitoa kadi kwa wanachama 19 ambao waliamua kujiunga na chama hicho jana. Hongera sana kwa kujinga na Chama Cha Mapinduzi, umechukua maamuzi sahihi.
Chukua Laki moja hii iwasaidie kama chama hapa Kagera kwenye mradi wenu wa ujenzi kwa kiwanja mlichoniambia kuwa mnacho. Alisema na kukabidhi kiasi hicho cha fedha, Mbunge, Dr. Mary Mwanjelwa jana eneo la Kagera kata ya Ilomba Jijini Mbeya. Wasanii nao walipatiwa Tsh.50,000/= baada ya kuimba vizuri na kuomba kuendelzwa vipaji vyao. Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa, akisikiliza risala katika tawi la Tonya, kata ya Ilomba alikofika kuzindua kijiwe cha vijana wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), ambao wanajishughulisha na usafirishaji wa abiria kutumia pikipiki (bodaboda).
KUONA PICHA
ZAIDI GONGA LINK HIYO HAPO CHINI www.marymwanjelwa.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment