Naibu
Katibu Mkuu toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma HAB
Mkwizu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia
maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yanayotarajiwa kuanza Juni 16,
katikati ni Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Bi. Roxana
Kijazi toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na mwisho
kulia ni Mkrugenzi Msaidizi Idara ya Uchumi na Ushauri Kazi Bw. Hassan
Kitenge.
Naibu
Katibu Mkuu toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma HAB
Mkwizu (kulia) akisistiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
mapema hii leo jijini Dar es Salaam juu ya maadhimisho ya siku ya
utumishi wa umma yanayotarajia kuanza tarehe16 Juni, kushoto ni
Mkurugenzi Idara ya Habari assah Mwambene.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu toka
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu (hayupo
pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya
Siku ya Utumishi wa Umma yanayotarajiwa kuanza Juni 16 jijini Dar es
Salaam.
Zaidi
ya Taasisi 30 za Serikali hapa nchini zinatarajia kushiriki katika
maonesho ya wiki moja ya utumishi wa Umma yanayotarajiwa kufanyika
kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar
es Salaam.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu wakati akizungumza na
waandishi wa habari juu ya kukamilika kwa maandalizi hayo.
Mkwizu alisema maadhimisho
hayo ambayo huratibiwa na ofisi yake yatafunguliwa rasmi na Waziri wa
Nchi ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Hawa Ghasia na
kuambatana na uoneshaji wa kazi mbalimbali za Taasisi za Serikali
wanazozifanya kila mwaka kwa lengo la kutathmini kazi zinazofanywa na
sekta hiyo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Kuadhimisha
siku hii kutakuwa na kongamano la siku mbili litakalojadili miaka
hamsini ya Muungano katika Utumishi wa Umma ambalo litafanyika kuanzia
tarehe 19 hadi 20 Juni katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kusimamiwa na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue”, alisema Bw. Mkwizu
Aidha
Bw. Mkwizu pia alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika
viwanja vya Mnazi mmoja ili kupata huduma na kutoa maoni juu ya kazi
mbalimbali zinazofanywa na Taasisi za Serikali.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‶Mkataba
wa Msingi na Kanuni za Utumishi wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya
kuimarisha utawala bora na Uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa Uwazi″
Kilele
cha Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka tarehe 23 Juni kama
ilivyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) mwaka 1994
katika mkutano wa Mawaziri wa Utumishi wa Umma barani Afrika uliofanyika
nchini Morroco.
……………………………………….
Na Eliphace Marwa -MAELEZO
0 comments:
Post a Comment