MASHABIKI
na wapenzi wa soka Brazil jana waliingiwa hofu kufuatia mshambuliaji
wao nyota, Neymar kukaa chini mazoezini akiugulia maumivu ya kifundo cha
mguu na kuzua hofu juu ya uimara wake keuelekea Kombe la Dunia.
Nyota
huyo wa Barcelona aliumia enka wakati wa mazoezi Selecao nje ya Rio de
Janeiro na kumlazimisha kupata huduma ya kwanza uwanjani.
Hata
hivyo, baada ya dakika kadhaa za kutibiwa, mchezaji huyo ambaye
amepamba bang la tangazo la Kombe la Dunia mwaka huu, aliinuka na
kuendelea na mazoezi.
Nafuu:
Neymar aliinuka baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na kurudi kuendelea
na mazoezi, kujiandaa na mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia keshokutwa
0 comments:
Post a Comment