Saturday 19 March 2016

ENGLAND - TIMU YA 4 HUENDA ISICHEZE UEFA CHAMPIONZ LIGI!

 ENDAPO Liverpool na Manchester City watatwaa Makombe huko Ulaya Msimu huu basi Timu itakayomaliza Nafasi ya 4 kwenye BPL, Ligi Kuu England, haitashiriki UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao kama ilivyo desturi.

Badala yake, Timu hiyo ya 4 itapelekwa kucheza UEFA EUROPA LIGI.
Hali hiyo inatokana na Kanuni za UEFA ambazo zinataka kila Mwanachama wake asiwe na zaidi ya Timu 5 kwenye UCL kwa Msimu wa 2016/17.
Hii inamaanisha kuwa endapo Man City, ambayo sasa ipo Robo Fainali, itatwaa Kombe la UCL na Liverpool kubeba EUROPA LIGI Timu hizo moja kwa moja zitacheza UCL Msimu ujao pamoja na Timu 3 za BPL.
Hivyo England tayari itakuwa na Timu 5 kwenye UCL na itabidi ile Timu ya Nafasi ya 4 kwenye BPL, ambayo kawaida hucheza UCL, ipelekwe EUROPA LIGI.
Lakini ikiwa City na Liverpool zitabeba Makombe ya Ulaya na pia kumaliza kwenye 4 Bora ya BPL, basi zile Timu 4 za juu za BPL zitacheza UCL kama kawaida.
Kwa sasa, kwa mujibu wa UEFA, Bingwa wa EUROPA LIGI Msimu unaofuatia hucheza UCL.

0 comments: