Tuesday 22 March 2016

FIFA kuchunguza Beckenbauer, 5 wengine


Image copyrightAP
Image captionBeckenbauer na wengine 5 kuchungwa na FIFA
Aliyekuwa Nahodha na kisha kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyotwaa kombe la dunia Franz Beckenbauer ametajwa katika orodha ya watuhumiwa 6 wanaoshukiwa kutoa hongo kununua kombe la dunia la mwaka wa 2006 huko Ujerumani.
Kamati ya maadili ya FIFA imetoa orodha wa watu 6 waliongoza kampeini hiyo ya kutwaa uwenyeji wa kombe la dunia.
Shirikisho la soka la Ujerumani lilipasua mbarika lilipofichua ripoti ya upelelezi ambayo ilimpelekea Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani kukiri kuwa alifanya makosa wakati wa kuwania zabuni ya wenyeji wa kombe hilo la dunia.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani wakati huo iliishinda Afrika Kusini kwa kura moja pekee.
Image copyrightREUTERS
Image captionMnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani ilipata kura 12 dhidi ya 11 za Afrika Kusini katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2000.
Orodha kamili
  1. Franz Beckenbauer
  2. Wolfgang Niersbach
  3. Helmut Sandrock
  4. Theo Zwanziger
  5. Horst Schmidt
  6. Stefan Hans

0 comments: