Tuesday 22 March 2016

Rubani wa Ukraine jela miaka 22 Urusi kwa kosa la .......?


Image copyrightAFP
Image captionRubani wa Ukraine jela miaka 22 Urusi

Rubani kutoka Ukraine anayetuhumiwa kwa mauaji ya wanahabari wawili kutoka Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani.
Nadiya Savchenko alipatikana na hatia ya kufyatua makombora yaliyowauwa wanahabari hao waliokuwa wakipeperusha habari kutoka eneo la vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga wanaoaminika kuungwa mkono na Urusi.
Kisa hicho kilitokea mwezi juni mwaka wa 2014.
Savchenko aliangua kicheko punde baada ya majaji hao kumaliza kusoma hukumu yao.
Alianza kuimba nyimbo za kitamaduni za kizalendo kama njia yake ya kupinga uamuzi huo.
Savchenko alikanusha madai dhidi yake.

Image copyright 
Image captionNadiya Savchenko alipatikana na hatia ya kufyatua makombora yaliyowauwa wanahabari 2 wa Urusi

Mara baada ya hukumu hiyo kutolewarais wa Ukraine Petro Poroshenko alipuzilia mbali uhalali wake na kusema kuwa yuko tayari kubadilisha rubani huyo shupavu na wanajeshi wawili wa Urusi waliokamatwa.
Aidha waziri wa maswala ya kigeni wa Ukraine aliahidi kuendelea na harakati za kutafuta uhuru wa rubani huyo.
Kulitokea makabiliano baada ya mashabiki wa rubani huyo kujaribu kupeperusha bendera ya Ukraine ndani ya mahakama.
Kiongozi wa mashtaka alisema kuwa bi Savchenko alikuwa na chuki sana dhidi ya Urusi na hiyo ndiyo iliyompelekea kuwashambulia waandishi habari hao,.ambao hawakuwa wamejihami.
Kesi hiyo iliendeshwa katika mji wa mpakani wa Donetsk.

0 comments: