Sunday 20 March 2016

KASI ya Rais Magufuli unawaka Kila kona...yafanya MADC wasikae ofisini ona hapa

Mkuu wa wilaya ya Moshi.Mhe.Novatus Makunga akiwa anaongoza vyombo vya ulinzi na usalama vya wilaya hiyo kuwasaka na kuwakamata watengenezaji wa Pombe haramu ya gongo inayosemekana kuleta maafa makubwa kwa wananchi hasa vijana wakipoteza nguvu kazi kubwa kwa kuathirika na pombe hiyo...Masama Blog ilimuhoji Mhe.Makunga naye alikuwa na haya ya Kusema
.'''............Ndugu yangu hii ni Operesheni tokomeza gongo katika msitu wa Rau.Kwa muda mrefu limekuwa likitumika kama viwanda vya kuchemshia pombe haramu ya gongo.Siku ya kwanza tulikamata lita 300.Lakini mwishoni mwa wiki mitambo mitano na lita 100.Katika hatua ya ajabu watengeneza gongo walijikusanya na kuanza mapigano na vyombo vya dola.Tunaendelea kuwasaka.......''Alisema DC Makunga.

0 comments: