Costa Rica wakishangilia ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Italia.
Imechapishwa Juni 20, 2014 saa 3:00 usiku
TIMU
yaTaifa ya Italia maarufu kama Azzuri imeangukia pua usiku huu katika
mchezo wa kombe la dunia kundi D baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0
dhidi ya Costa Rica.
Costa Rica wamepata ushindi wa pili katika kundi lao kwani mchezo w aufunguzi waliwafunga Uruguay mabao 3-1.
Kwa matokoe hayo, Costa Rica wamefuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 tangu mwaka 1958.
Bao pekee la Costa Rica limefungwa na Bryan Ruiz katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.
Bryan Ruiz akishangilia bao lake katika kipindi cha kwanza.
Ruiz akiunganisha kwa kicha mpira wa krosi na kufunga bao lake, huku kipa wa Italia Gianluigi Buffon akiwa hana la kufanya.
Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vya wachezaji. Alama ni chini ya 10.
Kikosi cha Italia (4-3-3):
Buffon 6; Abate 5, Barzagli 5.5, Chiellini 4, Darmian 4.5; Motta 5
(Cassano 45mins 6), Pirlo 6.5, De Rossi 5.5; Candreva 6 (Insigne 56mins
6), Balotelli 4.5, Marchisio 5 (Cerci 69mins 6) .
Kadi ya njano: Balotelli
Kikosi cha COSTA RICA (3-4-3): Navas 7.5; Duarte 7.5, Gonzalez 7, Umana 6.5; Gamboa 7, Borges 7, Tejeda 7 (Cubero 67mins 6.5), Diaz 7; Ruiz 7.5 (Brenes 81mins 6) , Campbell 7.5 (Urena 74mins 6.5), Bolanos 8. Mfungaji wa Goli: Ruiz 44 Mwamuzi: E Ossis (CHI) 5 Mchezaji bora wa mechi: Christian Bolanos

Kwa matokeo haya England kama tayari
wameshatupwa nje ya kombe la dunia, huku Italia na Uruguay watakuwa
wanagombania nafasi moja ya kundi D wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment