Friday 6 June 2014

BAADA YA PICHA ZA MH KOMBA ZA MAHABA KUSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII ADAI ZIME TENGENEZWA.


    Default


  1. PICHA za Capt. Komba zenye utata zasambazwa kwenye mitandao ya kijamii!





    Picha zinazomwonyesha mh. Captain John Komba zenye mapozi tofauti na mabinti tofauti zimeanza kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania.

    Kuna picha nyingine nyingi lakini kutokana na maadili hatuwezi kuziweka hadharani; hizi ni baadhi tu

    =======
    UTETEZI WA KOMBA:

    Kuhusiana na hizi picha 2 zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuznia asubuhi ya leo, zikimuonyesha Mheshimiwa Mbunge huyo wa CCM Kapteni John Komba akiwa kwenye mahaba na Mwanadada mmoja anayeishi Kinondoni.
    Mbunge huyo amesema kwamba picha hizi zimetengenezwa na maadui wake wa kisiasa na kwamba yeye sio Kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo.

    Kapteni Komba amesema kwamba anawakaribisha wataalamu wa Picha na Mitandao kutihibitisha ukweli wa picha hizo zinazoonyesha Mwana-Dada akiwa na kipande cha khanga tu huku Mbunge huyo akiwa pembeni yake akionyesha kutokuwepo kabisa kwenye Mahaba yanayotakiwa kuwa yanaendelea baina yao.

    Mbunge huyo ameuliza zaidi iweje awe kwenye mapenzi kama picha zinavyo onyesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa na khanga tu?

    Kapteni Komba amesema kwamba kama kweli Taifa hili limefikia hapa pa kuchafuana namna hii kisa mitizamo tofauti ya kisiasa ya namna ya kuongoza Taifa letu basi kama Taifa tumefikia pabaya sana.

    Mbunge huyo amemalizia kwa kusema kwamba wale wote wanaomuamini kama Kiongozi shupavu wa Taifa, wasikatishwe tamaa na wajinga wachache wenye mawazo ya kitumwa ambao wanadhani wanaweza kummaliza kisiasa kwa kumtengenezea picha chafu kama hizi picha 2 za leo!

0 comments: