Monday 19 May 2014

MATUKIO KATIKA PICHA YA WAZIRI MKUU MHE. PINDA MJINI DODOMA

PG4A9685 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kwa Waandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusu  zao la zabibu wakati walipotembelea shamba lake lililopo zuzu mjini Dodoma Mei 18, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A9725 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr.Mary Nagu, Bungeni mjini Dodoma Mei 19 , 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A9818 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na ujumbe  wa Kampuni ya  British American Tobacco, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Mei 19, 2014.Kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika mashariki, Ernest Leroux, Watatu kulia ni Mkurugenzi wa Afrika ya Mashariki na kati, Jerry Gilbert na kushoto ni Connie Anyika. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage, Teddy Mapunda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NA Rais Kikwete akutana na Viongozi wa MEWATA Ikulu DSM

D92A4105 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania(MEWATA) baada ya kukutana na kufanya nao mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro).

0 comments: