Monday 19 May 2014

MASCHERANO: ‘HIMAYA YA BARCA IMEKWISHA!’

MASCHERANOMCHEZAJI wa Barcelona mwenye asili ya Argentina, Javier Mascherano, ameungama kuwa zile enzi za Barcelona kutawala Soka la Spain na Ulaya sasa zimekwisha.
Huku akiwa kimya kuzungumzia hatima yake mwenyewe, Mascherano amesema Barca baada kupoteza Ubingwa wa La Liga na kuwaruhusu Atletico Madrid kupata Sare na Ubingwa ndani ya Nou Camp Juzi Jumamosi, Klabu hiyo sasa inapaswa kujijenga upya.
Mbali ya kuukosa Ubingwa huo, Barca pia ilitolewa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenye Robo Fainali na Atletico Madrid na pia kushindwa na Real Madrid kwenye Fainali ya Copa del Rey.
Hii ni mara ya kwanza kwa Barca kutoka mikono mitupu katika Msimu tangu 2007/08.
Mascherano anaamini Msimu huu ulidhihirisha ile himaya yao ya kutawala imekwisha na sasa inabidi ijijenge upya na tayari Kocha Tata Gerardo Martino ameshatangaza kuachia ngazi.
Mascherano ametamka wakati akiongea na Barca TV: “Kitu ambacho sio muhimu ni hatima ya Mascherano, Barcelona ndio muhimu. Ile himaya imekwisha! Klabu lazima iamue na mabadiliko yafanyike na tukubali Msimu huu haukuwa mzuri!”

0 comments: