Monday 19 May 2014

AZAM FC YAWAITA YANGA WAKAWACHUKUE BOCCO, NDUGU WA KIPRE



Uongozi wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam FC, umewaita mezani Yanga waende kufanya mazungumzo kuhusiana na wachezaji wake wawili, John Bocco pamoja na Kipre Balou kujiunga na kikosi hicho cha Jangwani.

Bocco na Balou wameingia katika rada za Yanga kufuatia ripoti ya aliyekuwa kocha wao, Hans van Der Pluijm kuutaka uongozi wa timu hiyo kusajili mshambuliaji ambapo Bocco amekuwa chaguo namba moja katika klabu hiyo huku Balou akitafutwa ili azibe pengo lililoachwa na Frank Domayo.

Bocco na Balou wote wana mikataba ya kuitumikia Azam kwa miaka mitatu inayokuja, hivyo kama Yanga itakuwa inawahitaji wachezaji hao, inabidi ivunje mikataba yao.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Msemaji wa Azam FC, Jaffari Idd, alisema wamesikia kuwa Yanga inawataka wachezaji wao hao, akasisitiza kuwa wao hawana pingamizi lolote na wanawaita mezani kufanya mazungumzo kama watakuwa tayari kuvunja mikataba waliyonayo.
“Hatuwezi kuwazuia Yanga kuwataka wachezaji wetu na tunawaambia waje tufanye mazungumzo na kama wapo tayari kuvunja mikataba ya wachezaji hao tutakuwa radhi kuwaruhusu,” alisema Idd.

0 comments: