Tuesday, 12 November 2013

ROBIN VAN PERSIE AZIKOSA MECH ZA HOLLAND NAENDTNER ATAKIWA NA DENMARK KUHAMA ARSENAL!

RVP-MAKOFI_JUUKAMBI ya Holland imethibitisha kuwa Straika wa Manchester United Robin van Persie ana maumivu na hivyo kuzikosa Mechi za Nchi hiyo na huko Denmark, Kocha Mkuu amemtaka Straika wa Arsenal Nicklas Bendtner aihame Klabu yake.

SOMA  HAPA UPATE UHONDO ZAIDI:

ROBIN VAN PERSIE AZIKOSA MECHI ZA HOLLAND
KAMBI ya Holland imethibitisha kuwa Straika wa Manchester United Robin van Persie ana maumivu ya Kidole cha Mguuni na pia kwenye Nyonga na hivyo hatakuwa fiti kucheza Mechi za Kirafiki za Nchi hiyo baadae Wiki hii dhidi ya Japan na Colombia.
Jumapili iliyopita, Van Persie alicheza Dakika 85 za Mechi ya Klabu yake walipoifunga Arsenal Bao 1-0 huku yeye ndie Mfungaji wa Bao hilo.
Ikiwa maumivu ya Staa huyo yataendelea anaweza kuikosa Mechi ijayo ya Man United ya Ligi Kuu England Ugenini na Cardiff City hapo Jumapili Novemba 24.
Baada ya Mechi hiyo zitafuata Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Bayer Leverkusen, kisha Mechi za Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham na Everton.

BENDTNER ATAKIWA KUHAMA ARSENAL
Straika wa Denmark Nicklas Bendtner ameambiwa na Kocha wa Nchi hiyo, Morten Olsen, aihameBENDTNER_na_CHUPI Arsenal kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari.
Bendtner, mwenye Miaka 25, alitarajiwa kuihama Arsenal kabla Msimu huu kuanza baada ya kuwa kwa Mkopo huko Sunderland na Juventus katika Misimu miwili iliyopita lakini Arsenal ikamtaka abaki.
Bendtner, ambae alijiunga na Arsenal toka akiwa na Miaka 16 akitokea FC Copenhagen, Msimu huu amecheza Mechi 7 za Arsenal lakini hajafunga na Bao zake pekee Msimu huu ni zile alizoifungia Denmark Bao mbili walipotoka Sare ya 2-2 na Italy kwenye Mechi ya Kombe la Dunia.
Na Kocha Olsen, ambae anahisi Bendtner anadumazwa huko Arsenal, amesema: “Bendtner alitufungia Goli mbili safi lakini kwenye Mechi ile alionyesha udhaifu na hilo linakuja tu kwa sababu ya kukosa kucheza Mechi mfululizo. Na kwa sababu hiyo tu ni lazima atafute Klabu nyingine. Wanasoka wanataka kucheza Soka!”

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 23 Novemba
1545 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Southampton
1800 Fulham v Swansea City
1800 Hull City v Crystal Palace
1800 Newcastle United v Norwich City
1800 Stoke City v Sunderland
2030 West Ham United v Chelsea
Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United
Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa
  
 Kwahisani ya soka inbongoblog
Tuesday, 12 November 2013 17:05

0 comments: