Tuesday, 12 November 2013

YANGA YAKANUSHA KUMCHUKUA HALL, KUMBWAGA BRANDTS!!

WASISITIZA: BRANDTS YUPO, ATAREJEA NOVEMBA 24 BAADA LIKIZO!

AKIREJEA, KUITAYARISHA TIMU KUIVAA SIMBA ‘NANI MTANI JEMBE’ DESEMBA 14!!

YANGA-BIN_KLEIB_n_BRANDTSMABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, leo imekanusha vikali taarifa zilizozagaa kuwa wapo mbioni kumchukua aliekuwa Kocha wa Azam FC, Stewart Hall, na kusisitiza kuwa Kocha wao Ernie Brandts bado yupo na ataendelea na kazi yake.AZAM_FC_PLAYERS-STEWART_HALL
Mbali ya kukanusha kutaka kumchukua Hall, anaetoka Uingereza na ambae hivi Juzi aliondolewa kuifundisha Azam FC, Yanga pia imesisitiza haijawahi kufanya mazungumzo na Kocha huyo.
Yanga imefafanua kuwa Brandts, ambae amemudu kuifanya Yanga imalize Raundi ya Kwanza ya Ligi Kuu Vodacom ikiwa kileleni,  kwa sasa yupo Likizo ya Wiki mbili ambayo pia Wachezaji wamepewa na Kocha huyo anatarajiwa kurejea Nchini Novemba 24 na Siku inayofuatia yeye na Kikosi chake wataanza Mazoezi kwa ajili ya mchezo wa Hisani, Nani Mtani Jembe, dhidi ya Simba utakaochezwa Desemba 14.
Taarifa hiyo ya Yanga ilisisitiza uvumi huu ulikuwa na lengo la kutaka kuwavuruga ili wasifanye vizuri kwenye Raundi ifuatayo ya Ligi na pia Mashindano ya Kimataifa.
Ligi Kuu Vodacom itaanza Raundi ya Pili hapo Januari 25.

LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Young Africans
13
8
4
1
31
11
20
28
2
Azam FC
13
7
6
0
23
10
13
27
3
Mbeya City
13
7
6
0
20
11
9
27
4
Simba SC
13
6
6
1
26
13
13
24
5
Kagera Sugar
13
5
5
3
15
10
3
20
6
Mtibwa Sugar
13
5
5
3
19
17
2
20
7
Ruvu Shootings
13
4
5
4
15
15
0
17
8
Coastal Union
13
3
7
3
10
7
3
16
9
JKT Ruvu
13
5
0
8
10
16
-6
15
10
Rhino Rangers
12
2
4
6
9
16
-7
10
11
JKT Oljoro
13
2
4
7
9
19
-10
10
12
Ashanti United
13
2
4
7
12
24
-12
10
13
Tanzania Prisons
12
1
5
6
6
16
-10
8
14
Mgambo JKT
13
1
3
9
3
23
-20
6

RATIBA
RAUNDI YA PILI
25 Januari 2014
Ashanti United v Yanga
Azam FC v Mtibwa Sugar
Coastal Union v JKT Oljoro
Kagera Sugar v Mbeya City
Tanzania Prisons v Ruvu Shootings
JKT Ruvu v Mgambo JKT
Simba v Rhino Rangers

0 comments: