Kamati
ya msiba ya mwanamuziki Albert Mangwea, imeleta taarifa kwamba mwili wa
Ndugu yetu Albert Mangwea hautoweza kufika siku ya jumapili ya tarehe
2/ 06/2013 kama ilivyo taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu
zilizokuwa nje ya uwezo wetu.
Kwa
sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu
waliopo nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo
tutawafahamisha zaidi.
Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu kwa hili.
0 comments:
Post a Comment