Mwanamke Mery Mbosa anayeishi kama mkimbizi baada ya kunusurika mara kadhaa kuchinjwa na mtalaka wake. |
========================================
Na Gustav Chahe, Iringa
MAMA mmoja
mkazi wa Itunundu – Pawaga katika Mkoa wa Iringa Mery Mbosa anaishi kama
digidigi baada ya kunusurika mara kadhaa kuchinjwa na mtalaka wake na
kulazimika kuhama kijiji kwa ajili ya kunusuru maisha.
Akiongea
na mtandao huu jana, Bi Mbosa alisema maisha yake yapo hatarini
kutokana na kuvamiwa na mtalaka wake mara kadhaa akiwa nyumbani na
kumuumiza.
Alisema
alilazimika kutalakiana baada ya mwanamume huyo kuwa mkorofi kiasi cha
kupigwa, kutokuwa huru kutumia mazao ambayo walilima wote na hata
kutokuwa huru kuongea na watu hata kama ni ndugu zake kwa madai kuwa ni
wivu wa kimapenzi.
Alisema
mtalaka wake amegeuka kuwa mnyama na kufika nyumbani kwake usiku wa
manane na pindi anapokuta mlango umefungwa huanza kurusha mawe
madirishani huku akitaka kuvunja mlango ili kuingia kumdhuru.
Amemtaja
mtalaka wake kuwa ni Phabiani Msilamgunda ambaye miezi ya hivi karibuni
alikutana na ye njiani akielekea shambani akamvamia akiwa na kisu kwa
kutaka kumchinja na kuokolewa na watu ambao walikuwa jirani.
“Ilikuwa
23 Machi mwaka huu nilikuwa nikielekea shambani nikakutana na mtalaka
wangu akiwa na kisu mkononi akanivamia huku akisema nakuchinja laeo
lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na watu jirani wakaniokoa vinginevyo
ningekuwa marehemu.
“Lakini
hata hivyo amekuwa akimtukana hata mama yangu mzazi (mama mkwe) akitaka
kupiga pia na kila wakati nimekuwa nikishtaki hadi ofisi zinanichoka
pamoja na kuwa ninapokelewa na akiitwa haendi kwa sababu amekuwa mbabe”
alisema bi Mbosa.
Hata
hivyo Mbosa alisema kuwa aliwahi kupigwa na kuumizwa vibaya na
kulazimika kushtaki mahakamani japo kuwa hukumu ilivyotolewa haikuwa ya
haki na kuhatarisha zaidi maisha yake.
“Nilipigwa
na kuumizwa vibaya kesi ikapelekwa mahakamani lakini hukumu
ilivyotolewa haikuwa ya haki kwangu na baada ya hukumu maisha yangu
yamekuwa ni ya hatari zaidi” alisema.
Kwa
mujibu wa maelezo ya wananchi wa kijiji hicho ambao wameeleza
kushuhudia mama huyo akinusurika kuuawa na jinsi maisha yake yanavyozidi
kuwa mabaya, walisema kiburi cha Msilamgunda kinatokana na dada yake
ambaye ni diwani wa viti maalum (CCM).
Gazeti
hili limebaini kesi ambayo mama huyo hajaridhika na hukumu ni Jinai No.
22/2013, mshitakiwa Phabiani Msilamgunda ambayo ilitolewa hukumu Mei 21
Mwaka huu.
Imeelezwa
kuwa katika utoaji huku hiyo hakimu aliyetajwa kwa jina moja la Masuwe
alimtaka mtuhumiwa alipoe faini ya shilingi laki mbili pamoja na gharama
ya kesi shilingi 45 elfu jambo ambalo lilifanyika hivyo na mtuhuhumiwa
kuwa huru kwa vitisho kuwa lazima ammalize mwanamke huyo.
Pamoja
na kutokuridhika na hukumu iliyotolewa, Mkuu wa kituo cha Polisi cha
Pawaga Fedrick Nyavilwe anatuhumiwa kumdhurumu mama huyo na kuiomba
serikali kumsaidia ili aishi kama wanavyoishi wananchi wengine.
Nyavilwe
anatuhumiwa kumdhurumu mwanamke huyo mbegu ya mpunga na kumfanya kuwa
mtumwa kwa kukosa chakula bila kujua hatima ya maisha yake.
“Baada
ya hukumu nilikwenda shambani nilikokuwa ninaanda mbegu ya mpunga kwa
ajili ya kupanda nikakuta watu wananing’oa, nilipouliza walisema
wametumwa na Mkuu wa kituo cha polisi. Hivi sasa naishi kama ndege
jamani sijui nitakula nini kwa sababu hata mashamba niliyokuwa nalima
nilinyang’anywa na mbegu niliyokuwa nimeandaa kwa ajili ya kupanda
polisi wameninyang’anya” alisema.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu kwa ajili ya kutolea maelezo, Veronica Msilamgunda
ambaye ni ndugu na Phabian Msilamgunda alisema hawezi kuzungumza
chochote kwa kuwa yupo kwenye mkutano.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Malinga alipotafutwa kwa
ajili ya ufafanuzi Alikiri kuwa mama huyo ni mhanga mkubwa na anaishi
kama mkimbizi kwa hofu ya kuuawa.
“Nalijua
sana hilo na ninashukuru kwa kuwa umenitafuta ili nikueleze. Maisha ya
huyo mama hatuji yataishia wapi kwa sababu hali ilivyo kwa sasa ni ngumu
na anaishi kama mkimbizi.
“Hata
akiwa sehemu yenye ulinzi anaona kama hakuna ulinzi kwa sababu ya kile
anchofanyiwa. Kiujumla hata sisi viongozi wa kijiji tunaishi kwa mashaka
kwa sababu tunatishiwa kuuawa tunapotaka kutafutas suluhu ya huyo mama.
Huyu mwanaume tunashindwea kuelewa kama ni mtu wa kawaida maana
amegeuka kuwa kamas samba” alismea Malinga.
Hata
hivyo alisema anaomba kwa watu wanaoweza kumsaidia mama huyo kupata
hifadhi ili aondokane na maisha ya kuishi kama digidigi kule kijijini.
Na Gustav Chahe, Iringa
Kwa msaada waFrancisgodwinblog
0 comments:
Post a Comment