Wakuu wa Iraq wanasema
wamegundua njama ya al-Qaeda kutaka kutumia silaha za kemikali nchini
Iraq na kuzisafirisha kwa magendo hadi Ulaya na Marekani.
Msemaji wa wizara ya ulinzi, Mohammad al-Askari,
alisema idara ya usalama ya jeshi imegundua karakana tatu za
kutengeneza kemikali hizo, pamoja na kemikali ya kuharibu neva.
Bwana al-Askari aliiambia televisheni ya Iraq kwamba wanaume watano walikamatwa baada ya kuchunguzwa kwa miezi mitatu.
Wote walikiri makosa, alisema.
0 comments:
Post a Comment